Tujikite zaidi kwenye ukweli na tupunguze zile propaganda za soka, kwanini hatutaki kuuzungumza ukweli juu ya kufanikiwa kwa mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ baada ya kuelekeza nguvu zake ndani ya Yanga SC.

Kabla ya Ghalib kuingia Yanga, mkumbuke vizuri klabu hiyo ilikuwa kwenye mazingira yapi, ilikuwa kwenye hali mbaya ya kifedha timu ilikuwa ikihahaa kupata japo hata ule usafiri tu kufika kwenye michezo yake. Klabu hii ilifikia wakati wa kuchangishana na kuliita BAKULI la MCHONGO.

Ghalib Said anaingia Yanga na kwenda kuyaondoa yote hayo sema tu tunapenda kusifia tuvipendavyo. GSM kukaa kwao hapo Yanga imeenda kubadilisha kila kitu, leo hii Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfurulizo, Yanga ililipa kisasi cha mabao 5 kwZ mtani lakini kubwa zaidi ni kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho.

Yanga SC imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho na kuifunga timu ngumu ya USM Alger nchini Algeria pamoja na kulikosa kombe Lakini alama imewekwa. Kama inasifiwa timu iliyocheza robo tatu za Ligi ya mabingwa, vipi Ghalib Said ambaye kuwepo kwake tu Yanga SC imeshaingia Robo fainali na pia inatazamiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za vilabu.

Ukizungumza mambo kama haya watatokea Machawa Kisha kutumia account fake kuupondo ukweli huu. Katika ukweli tuseme kama aliwahi kusifiwa mtu kufanya vyema basi Ghalib Said Mohamed na watu wao nao tuwapongeze. Ukweli ni kwamba, GSM wameubadilisha mpira wameipa Yanga thamani ya KIMATAIFA hakuna asiyelijua hili.

Wacha ninyamaze sema wale wasemaji wapunguza kauli za Mtaani kuja kutumika kwenye taasisi kubwa zilizojaa watu wenye heshima zao. Itakushusha hata kama umesoma mpaka level ipi ya Elimu, tuchunge ndimi zetu.

SOMA ZAIDI: Karabaka Ni Dhahabu Iliyopo Simba Isiyotumika Vyema

1 Comment

  1. Pingback: Freddy Anahitaji Msaikolojia, Ana Tatizo Hili Kubwa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version