Aubin Kramo Kouamé(28) ni miongoni mwa majina ambayo Msimu huu wa mashindano unaomalizika mashabiki wa Simba na wadau wengi wa soka walitamani kumuona uwanjani, watu walitaka kuona ni kitu gani cha tofauti atapeleka ndani ya Msimbazi hasa katika eneo la ubunifu ambalo Timu inahitaji wachezaji wengi ili kuzalisha idadi kubwa ya magoli

Pale Ligi Kuu ya Ivory Coast ukitaja jina la Aubin Kramo basi utakuwa umetaja miongoni mwa majina ya wachezaji wachache sana wenye vipaji vikubwa sana ambao wamepita ndani ya Ligi hiyo, pale wamtambua Aubin Kramo kama mchezaji ambaye alipaswa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wapo Ulaya kama Karim Konate, Sankara Kalamoko na wengineo waliotoka pale

Kama ambavyo Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua walikuwa MVP wa Ligi Kuu ya Ivory Coast basi Aubin Kramo alifanya hivyo pia kwa Msimu wa Mwaka 2022-23, Kramo wakati anaingia Simba aliingia kama MVP wa Ligi Kuu y Ivory Coast na katika wakati ambao watu wanatamani kuona miguu yake inaleta kitu gani ndani ya uwanja basi ndio wakati ambao anapata majeraha

Majeraha ambayo amepata Aubin Kramo muda mwingi yamemuweka nje ya uwanja na Msimu huu unamalizika ikiwa Simba SC haijaona hata Robo ya Ubora wake aliotoka nao ndani ya Ivory Coast akiwa kama MVP! Hapa ukiacha Benchi jipya la Ufundi, Utamaduni, Ada ya Usajili, Wachezaji anaowakuta mchezaji husika na vitu vingine basi majeraha pia ni miongoni mwa vitu ambavyo hufanya mchezaji aonekane amefeli ndani ya Timu fulani

Binafsi bado naamini kama ambavyo nilishasema hapo awali AUBIN KRAMO KOUAMÉ ndio Usajili Bora ambao Simba walifanya katika Dirisha kubwa la Usajili lililopita ni vile majeraha yamefanya amekuwa nje muda mwingi kuliko uwanjani, kama Simba ingepata hata Robo Tatu ya Ubora wake ambao alitoa ndani ya Asec Mimosas basi kuna sehemu kubwa sana wangesogea kutokana na uwezo alionao

Simply! Mkataba wa Aubin Kramo unamalizika June 30 Mwaka 2025 na Kwakuwa Msimu mpya unaanza hivi karibuni basi tusubiri ataleta kitu gani ndani ya uwanja, pia kama yupo vizuri kurejea uwanjani na Simba wakabaki naye huenda basi wakapata kitu bora sana ambacho walihitaji kutoka kwenye ubongo na miguu yake.

SOMA ZAIDI: Al Ahly Na Maajabu Ya Jezi Namba 72 Kabla Ya Mechi

12 Comments

  1. Upande wangu mm naona aachwe tu tuangalie namna nyingine ya kupata mchezaji atakae onekana kwenye kiwanja na sio msimu mnzima majeruhi
    Inachosha anakula tu hela bila kuitendea kazi
    Enough it’s enough

    • Aachwe ili iweje,
      Unamuachaje MVP wewe c utakuwa mwehu..
      Msimu wote umemvumilia leo unataka kumuacha akiwa hata hajakufanyia lolote Zaid ya kumlipa mshahara…
      Ana kitu,ulivuta subra juu yake hvy wakat wa mavuno kwa huyo mwamba unakaribia

  2. Kwakuwa bado anamkataba na simba sivyema aondoke..inabidi abaki uenda akaleta matunda bora msimu ujao.
    #Nguvu moja

  3. Kramo ni Simba na Simba ni kramo…
    Msimu ujao watafute watu na huyo MVP awepo mbona boli litembee tu

  4. Kramo ni bora kuliko pacome kuliko Aziz ki kilicholeta shida no majeruhi tu kwakua anaendelea na mazoez sioni sababu yakumuacha anavitu vingi Sana vyakutupa na tunamdai… Umakini uwepo kweny usajili kuna majipu yakutumbua lakin sio kramo
    #nguvumoja

  5. Shida yetu Tanzania hatuna uvumilivu kramo ni fundi kila mwanasimba anatambua Hilo wanapaswa wampe muda amprove kile alichonacho I think tutamkubali tu

  6. kramo ni mchezaji mzuri sana injuries ni sehem ya maisha ya wachezaji mimi naona wanasimba tumpe muda kwa tulimsajili aje kuitumikia simba na sio kuja na kuondoka tumpe muda tuone uwezo wake ni mapema sana kumkatia tamaa mchezaji kama Aubin kramo
    #Nguvu moja

  7. Kama bench la ufundi na madaktari wamethibitisha kuwa yupo sawa kiafya ni bora aendelee kubaki kwa msimu mmoja pengin subra ikawalipa

  8. Mpaka mafuta on

    Wananchi tunasubiri gwaride kwa mkapa🔥🔥 sisi tuna pacome, aziz ki aucho wao wana nani??💚💛

  9. Pingback: Uso Wa Saido Ntibazonkiza Unazungumza Mengi

Leave A Reply


Exit mobile version