Ulikuwa ni ushindi muhimu kwa Simba SC na kuendelea kuwapa nafasi nzuri kwenye Ligi na kuendelea kuwapa Furaha mashabiki wao, ila kama ni msimu ambao hawatausahau kwa miaka hii ya karibuni basi ni msimu huu wamepata matokeo ila hawakuwa na mchezo mzuri, Singida Fountain Gate FC ni kama mtumbwi umezidiwa na maji wamepoteza mchezo wa tano mfululizo ndani Ya michezo sita hawajaambulia ushindi kwa muda mrefu sasa.

Kipindi cha kwanza, kilikuwa zaidi kwa Simba SC wakianza na Viungo wakabaji wawili Mzamiru Yassin n Fabrice Ngoma na kuwapa nafasi zaidi Chama, Ntibazonkiza na Kibu kuwa huru na kutengeneza nafasi ambapo waliweza kutengeneza nafasi nyingi zaidi ila matumizi yakawa sahihi kwa nafasi tatu tu, Simba SC walianzaje? 4-2-3-1 jambo ambalo walikuwa zaidi kwenye nusu Ya Singida FG muda mwingi wa kipindi cha kwanza, nini sababu ? Ni Singida FG kuamua kufunguka mapema sana mwa mchezo jambo ambalo lilipelekea wachezaji wengi wa Simba SC kuwa huru kucheza na kupiga pasi na kupelekea kuzaa magoli matatu.

Bado Simba SC walikuwa wazi sana hususa eneo la kati ya uwanja muda mwingi sana Fabrice Ngoma na Mzamiru Yassin walikuwa wakitoka kwenye maeneo yao na ilipelekea baadhi Ya uanzilishi wa mashambulizi kwa Singida FG kufanikiwa kupitia eneo ilo, Kwa Singida FG eneo lao la ulinzi ndiyo lilikuwa Active zaidi kwa kipindi cha kwanza huku Yusuph Kagoma akikosa msaidizi wa kukaba eneo la kati.

Kipindi cha pili kilikuwa upande wa Singida FG zaidi na kivipi wakifanikiwa? kwanza waliaamua kukimbia eneo kubwa la uwanja kuliko wachezaji wa Simba SC jambo ambalo liliwasaidia zaidi kumiliki mpira, pili walifanya “Press” Kwa nguvu sana na hiyo iliwanyima nafasi Simba SC kuwa huru kama kipindi cha kwanza, kitendo hicho kiliwapa presha wachezaji wa Simba SC na kupelekea kutotulia na mpira muda mrefu na tatu wakiamua kutumia mabeki wengi sana hususa eneo la pembeni walimtumia Amos Charles na Yahya Mbegu upande mmoja pamoja na Nicolas Gyan na Nicolaus Wadada upande wa pili.

Changamoto yao ilikuwa wapi ? Baada Ya kufanya “press” na kumiliki mpira maamuzi mengi hayakuwa sahihi kwao hususa kwenye eneo Lao la mwisho walikuwa wakipoteza mipira kwanini ? Walikuwa wakitumia zaidi wachezaji wenye asili ya kukaba na hata mabadiliko ya kuingia Thomas Ulimwengu na Kasengu Kazadi kidogo kulionyesha ishara Ya uoatikanaji bao.

1. Ayoub Lakred alikuwa na siku nzuri kiwanjani save tatu za Hatari
2. Chama ni kama alihitaji kutoka na Assist Leo ila wenzake walishindwa kutumia nafasi 4 alizotengeneza
3. Yusuph kagoma kwenye kiwango bora sana

Full Time || Simba SC 3-1 Singida Fountain Gate FC

SOMA ZAIDI: Kwanini Mdhamini Mmoja Timu 6 Ligi Moja?

2 Comments

  1. Pingback: FIFA SERIES 2024 Ni Michuano Gani? Na Inafanyikaje? - Kijiweni

  2. Pingback: Barua Ya Wazi Kwako Dickson Job “Big Brain Defender” - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version