Kama ni wakati kwetu na mambo kubadilika basi ni ili la timu zetu kuanza kujikwamua kwenye swala la kujenga nembo bora na jina bora la timu ambalo imekuwa rahisi kupata wadhamini wengi kwa muda mfupi, ndani ya Ligi kuu ya NBC kuna timu 16 na hakuna timu hata moja ambayo haina udhamini wowote kwani kuna udhamini wa kampuni tatu tofautia Azam TV, TBC na NBC Bank ambazo zinatoa hela kwa kila timu zote shiriki.

Tofauti ni kuwa nje ya udhamini rasmi wa Ligi nzima vilabu vingi vimejipatia wadhamini kadhaa kupitia ubora wa kikosi chao wanaonyesha uwanjani, vilabu zaidi ya 10 vinaudhamini kuanzia mmoja na zaidi na kama inavyojieleza kuwa vilabu vya Simba SC na Yanga SC ndiyo vilabu vyenye “Engagement” kubwa zaidi kuliko vilabu vyote nchini na hiyo imetokana na ukubwa wao kuanzia majina ya wachezaji wanaowamiliki na hata wafuasi wake pia kuwa wengi kuliko vilabu vyote nchini.

Ila usichokijua ni kuwa vilabu hivyo vimepitwa na klabu ya Singida Fountain Gate FC kuwa na wadhamini wengi kuliko wakubwa hao kutokana na ilo hii ndiyo orodha ya vilabu vyenye wadhamini wengi Ligi kuu ya NBC.

 

1.Singida Fountain Gate Fc

Makazi yake rasmi yalikuwa mkoani Singida kama jina lake linavyosomeka ila kwa sasa imebadilisha na kuwa inapatikana Mwanza. Hii ndiyo klabu yenye wadhamini wengi Ligi kuu ya NBC ikiwa na jumla ya wadhamini 9 wengi zaidi kuliko klabu yoyote ile.

Mdhamini mkuu wa klabu hiyo ni SportPesa huku wadhamini wengine wakiwa ni Haier, Azam TV, Coral Paints, Airtel, Vunjabei, Uhai, Nassco, Precision Air pamoja na Jet&Son ambao ni mdhamini wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo.

 

2.Simba Sc Tanzania

Kariakoo mtaa wa Msimbazi ndiyo makao rasmi ya klabu hiyo iliyo na zaidi ya miaka 80 tokea kuanzishwa kwake, imefanya makubwa sana nje na nchi na hiyo imefanya kutengeneza jina na kupata wafuasi wengi na wadhamini wakutosha, kwa sasa ina jumla ya wamiliki 8.

Mdhamini mkuu ni M-bet huku wadhamini wengine wakiwa ni Sandaland The only one ambaye anahusika na Jezi, Azam TV, Air Tanzania, MobiAd, MoXtra, Mo Assuarance pamoja na Pilsner Lager.

 

3.Yanga Sport Club

Ikiwa na miaka 89 tokea kuanzishwa kwake ikiwa maskani yake ni Dar es Salaam mitaa ya Jangwani ikiwa na jumla ya wadhamini 7 kutoka kampuni mbalimbali.

Mdhamini mkuu wa klabu hiyo ni SportPesa huku ikiwa na NIC kama mdhamini wa tuzo ya Mchezani bora wa mwezi, Haier, GSM, Azam TV, Hero pamoja na Whizmo kama mdhamini mkuu wa kikosi hicho kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

4.Coastal Union

Inaweza ikawa imekushangaza ila ndiyo klabu ya nne nchini kuwa na wadhamini wengi ikiwa na jumla ya wadhamini sita (6) ikiwa na maskani yake mkoani Tanga.

Mdhamini mkuu wa timu hiyo ni kampuni ya Elsewedy Cables huku wadhamini wengine wakiwa ni SleekSingh, Haier, K Security pamoja na Azam TV

 

5.Namungo Fc

Haina misimu mingi sana ila ni klabu ambayo kwa muda mfupi tu tokea ipande Ligi kuu ya NBC imefanikiwa kushiriki michuano ya Shirikisho Afrika CAFCC na kufuzu hatua ya makundi ambapi maskani yake ni mkoani Lindi ikiwa na jumla ya wadhamini watano (5) tu.

Mdhamini mkuu wa timu hiyo ni SportPesa huku ikiwa na wadhamini wengine ambao ni Azam TV, Coral Paints, Haier, Lodhia Industries pamoja na Swahili wote.

Hivyo ndivyo vilabu vyenye wadhamini wengi ndani ya Ligi kuu ya NBC ambapo masikio ya wengi ilikuwa ni ngumu kudhania kuwa Singida Fountain Gate FC ana wadhamini wengi kuliko Simba SC na Yanga SC ila tofauti kubwa ni kuwa Wadhamini wengi wanaoingia mkataba wa kuvidhamini vilabu hivyo wamekuwa wakisaini mikataba yenye thamani kubwa kuliko mikataba ambayo inasainiwa na wengine na hiyo ndiyo tofauti pekee tu, dhamani ya Simba SC na Yanga SC imebebwa na jina na ukubwa wao huku pia na ushiriki wao kwenye michuano ya Afrika.

SOMA ZAIDI: Ni Mwaka Wao Watachukua Tuzo Nyingi Sana Msimu Huu

1 Comment

  1. Pingback: Azam FC Mmetengeneza Ugonjwa Utakaosumbua Ligi Kuu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version