Kwa wawekezaji au unaweza kuwaita maafisa ubashiri mara nyingi hukumbana na kadhia ya mikeka kuchanika kutokana na kutofuatilia takwimu za timu wanazowekea ubashiri lakini pia na kutokufahamu timu za kuziepuka wakati wakiwa wanasuka mikeka yao ambayo wanaamini watashinda.

Timu ambazo tunakuwekea hapa ni zile ambazo wengi wamekutana na changamoto ya kuchaniwa mikeka kutokana na jinsi ambavyo zinakua zinacheza katika mechi zao bila kusahau kuwa mara nyingi hupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mechi hizi.

Kama unataka kushinda pesa kila wiki katika ubashiri basi nakuomba epuka timu hizi katika ubashiri:

Monaco na Celtic wanaingia katika orodha hii kama timu za kuziepuka unapokua unasuka mikeka yako ya ushindi na hii ni kwasababu katika mechi zao wanapokua wanacheza ugenini basi kuwa nao makini kwani kukuchania mikeka kwao ni suala la kawaida tu.

Valencia ilikua ni moja kati ya klabu ambayo wawekezaji wa mikeka walikua wanaitumia sana katika ubashiri wa mechi zao kutokana na kuwa na kikosi kizuri sana lakini kwa hivi sasa na haswa kwa msimu huu wamekua hawana kikosi kizuri kwa ushindani jambo ambalo ni wazi wanatakiwa kuepukwa katika ubashiri.

Rangers nao wanaingia katika orodha hii kwani mara nyingi huwa hawatabiriki leo wanaweza wakashinda kesho wakafungwa au wakapata sare jambo ambalo hukwamisha mikeka ya wawekezaji.

Vijana wa Diego Simeone yaani Atletico Madrid nao huwa wazinguaji sana katika mikeka kwani baadhi ya mechi zao wanaweza kuwa wa kwanza kufunga na kumiliki mchezo muda mrefu tun a baadae ukashangaa mechi ikaisha sare au wakafungwa.

Besiktas ilikua nayo ni moja ya timu kubwa zaidi katika ligi ya Uturuki lakini kwa sasa imekua timu ya hovyo sana kwa sababu wamekua na wakati mgumu sana katika ligi ya Uturuki na mimi nakushauri kuwaepuka katika mikeka yako.

Timu nyingine ambazo zinaingia katika orodha hii ni Pamoja na Borussia Dortmund, Sassuolo,

Galatasaray,Everton,AC Roma na timu nyingi zinazopatikana katika ligi ya English Championship.

SOMA ZAIDI: Nini Maana ya “GG in Both Halves” Katika Betting?

4 Comments

  1. Pingback: Mkeka Wa Leo Alhamis Wenye Timu 8 - Kijiweni

  2. Pingback: Mkeka Wa Leo Ijumaa Wa Kuianza Wikiendi Na Kibunda - Kijiweni

  3. Pingback: Mkeka Wa Leo Jumamosi Wa Uhakika - Kijiweni

  4. Pingback: Mkeka Wa Leo Jumanne Ushindi Wa Chaap - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version