Kiungo wa kati wa Arsenal Thomas Partey amefichua ni kwa jinsi gani kikosi cha Mikel Arteta kingekaribia mchezo wao ujao wa Premier League ambao ni dhidi ya wapinzani wao Manchester City.

Arsenal, wakiwa kileleni mwa jedwali la ligi tangu mwanzoni mwa msimu, taratibu wamepoteza kushikilia ubingwa.

Katika mchezo wao wa mwisho, The Gunners walifanikiwa kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Southampton na matokeo hayo yameifanya Manchester City kutawala mbio za ubingwa.

Manchester City wako pointi tano nyuma ya The Gunners lakini wana michezo miwili mkononi na ikiwa wataifunga Arsenal katika pambano lao la Jumatano huko Etihad, kikosi cha Pep Guardiola kitaibuka kidedea kushinda taji hilo tena.

Lakini Thomas Partey alisema Arsenal wako tayari kupambana hadi mwisho na watasafiri hadi Manchester wakiwa na mawazo ya kushinda mchezo huo.

“Nadhani kila kitu kinategemea sisi – lazima twende [City] tukiwa na mawazo ya kucheza soka…mwisho, lazima tujaribu na kushinda,” alisema, kulingana na Daily Mail.

Partey aliongeza: “Lazima tuichukulie kama mchezo kwa kuwa tunafanya kila kitu tulichofanya tangu mwanzo wa msimu na nina uhakika tunaweza kushinda ikiwa tutafanya hivyo. Hatuwezi kuweka vichwa vyetu chini kwa sababu sasa si wakati wa kuangusha vichwa. Ni lazima tuendelee kupambana.”

Leave A Reply


Exit mobile version