Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa Ali Hasan Mwinyi ulioko Tabora kutumika katika mechi za ligi baada ya kukidhi vigezo vya kikanuni baada ya kufanyiwa marekebisho wakati wanaufungia.

Taarifa hiyo kutoka kwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo inaeleza kuwa uwanja huo ulifungiwa baada ya eneo la kuchezea kutokidhi masharti ya kanuni na leseni lakini sasa umekaguliwa na kukidhi vigezo na masharti ya klabu baada ya marekebisho yaliyotakiwa kufanyika kutekelezwa kwa wakati.

Uwanja wa Ali Hasan unatumiwa na klabu ya Tabora United ambapo zamani ilikua inajulikana kama KITAYOSCE na kufunguliwa kwa uwanja huo ni fursa kwa wakazi wa Tabora kuziona klabu kubwa zikicheza na klabu yao ya Tabora na mchezo unaofata ni Tabora United dhidi ya Yanga katika dimba hilo hilo.

Kwa undani zaidi hii ni barua ya TFF:

 

Barua ya TFF ikizungumzia kufunguliwa kwa uwanja wa Tabora United.

Kwa taarifa zaidi za michezo unaweza kuendelea kusoma hapa.

1 Comment

  1. Pingback: CHAMA Na KAPAMA Wasimamishwa SIMBA - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version