Ikiwa leo ni Machi 31, 2023, vilabu vimeendelea kusaka nyota wapya kutoka timu kadha wa kadha ili kuimarisha vikosi vyao ili pia kujiweka sawa kujiandaa na msimu ujao ambapo ligi mbalimbali zinatarajia kuelekea ukingoni. Sasa hizi ni Tetesi za usajili kutoka kwa vyanzo vya habari duniani.

Chelsea wanataka kitita cha pauni milioni 70 kumuuza kiungo wa kati wa England Mason Mount, 24, licha ya kusalia na mwaka mmoja wa mwisho wa kandarasi yake. (Athletic)

Mount ana nia ya kujiunga na Bayern Munich na kuungana na meneja wake wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel. (Guardian)

Klabu ya Saudi Arabia Al Hilal inataka kumfanya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Mirror)

Lakini klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Inter Miami ina matumaini ya kumsajili Messi na kiungo wa kati wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets, 34, msimu ujao. (Sport)

West Ham huenda ikaachana na meneja wao David Moyes mwishoni mwa msimu huu, bila kujali kama klabu hiyo itaepuka kushushwa daraja. (90Min)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 36, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na AC Milan ambao utaendelea hadi 2024. (Fabrizio Romano)

AC Milan wamepewa ofa ya kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 28, kabla ya kuondoka Liverpool msimu huu mkataba wake utakapomalizika. (Calciomo)

Leave A Reply


Exit mobile version