Mshambulizi wa zamani wa Manchester United Andy Cole ameiambia klabu hiyo kupata msukumo kutokana na uhamisho wa Erling Haaland kwenda Uingereza na kumsajili Victor Osimhen.

Alisema Red Devils wanapaswa kunyakua fursa ya kumsajili Osimhen badala ya Harry Kane.

Manchester United wakiwa sokoni kusajili mshambuliaji wa kuisaidia kuwania mataji msimu ujao

Haaland amefunga zaidi ya mabao 40 akiwa na Manchester City katika msimu wake wa kwanza kwenye Premier League na Cole anaamini kuwa Manchester United inapaswa kutafuta kufanya makubaliano kama hayo.

“Harry Kane ana umri wa miaka 30 msimu ujao na Victor Osimhen kwa sasa ana umri wa miaka 24 na tayari amefanya mengi katika umri wake pia,” Cole aliiambia King Casino Bonus.

“Ikiwa Manchester United wanataka kulipa pauni milioni 100 kwa kijana wa miaka 24 au 30, lazima uangalie kwa muda mrefu. “

Leave A Reply


Exit mobile version