Kwanza kama Tanzania, tunapaswa kujipongeza kwa ukuaji wa soka letu hakika mpira wetu umekuwa sana tujipige kifua katika hilo. Lakini wanasema kwenye kila ongezeko la maendeleo ndivyo na majaribu yanaongeza tusikatishwe tamaa tuyafanye kuwa mtaji.

Vilabu vyetu vya Simba SC na Yanga SC vilikuwepo toka enzi na enzi, Yanga SC ikianza mwaka 1935 huku mwaka mmoja mbele Simba SC ikafuata mwaka 1936, itakuwa ngumu kusema hakuna Mtanzania ambaye hashabiki moja ya klabu hizo. Huyo atakuwa siyo mtu wa mpira pengine.

Katika ukuaji wa soka lakini tusisahau na hii mitandao ya kijamii nayo inakua kwa kasi, ongezeko ni kubwa na watu wameendelea kutumia, shida siyo unaitumiaje ila unautumia vipi mtandao wa kijamii. Nimeanza kuona baadhi ya wadau wa soka kupitia huu utani wa Simba na Yanga wanataka kuingiza chuki kupitia mpira, zipo lugha zisizofaa na wengine wanapandikiza chuki za wazi wazi.

Tuambiane kitu hapa kuwa duniani kote ukiona maendeleo ya mpira ujue nyuma yake wapo matajiri wamewekeza yaani wameingiza gharama zao kwamaana ya Pesa/Fedha Sasa itakuwa ngumu wewe mtu mmoja uje uvuruge hili.

Kama tumekubaliana kuondoka kwenye mpira wa MDOMONI na kuuleta MGUUNI hakuna haja ya kuenezeana chuki ni ngumu kumvumilia binadamu wa namna hiyo. Tangu na tangu, enzi na enzi nchi yetu inasifika kuwa kisiwa cha amani kwahiyo hatutakubali kuona mtu mmoja anataka kuivuruga amani yetu, hapo hatuko tayari.

Tumuogope mwanadamu ambaye yuko tayari kumkwamisha mwingine kwa maslahi yake binafsi au uchawa kazini ilimradi tu aonekane bora huku akiiteketeza familia ya mwingine.

Narudia tena, Tanzania mpira unakua, Soka lanazidi kupaa juu kwaiyo tusikubali kuharibu tunu hii Kwa kuondekeza Uchawa ilimradi tu usifiwe na Boss halafu upige pesa MCHONGO. Hiyo siyo sawa.

SOMA ZAIDI: Barua Kwa Waziri Ndumbaro Kuhusu Jezi Na Uzalendo

Leave A Reply


Exit mobile version