Wakati macho na masikio ya wengi hii leo ni kuona namna gani kama yataendelea maajabu ambayo yamekua yakijitokeza katika michuano ya mataifa barani Afrika huku mechi kubwa kadhaa zikipigwa lakini inayozungumzwa zaidi ni ya Tanzania dhidi ya DR Congo ambao ni mchezo wa mwisho kabisa hatua ya makundi kutoka kundi F.

Mchezo wa leo ambao kikanuni ni kwamba DR Congo yuko ugenini kwani mwenyeji wa mchezo huu ni Tanzania ambaye  yuko nyumbani katika uwanja wa Amadou Gon Coulibaly wenye uwezo wa kuingiza takribani watazamaji elfu ishirini.

Kila mmoja ana mtazamo wake juu ya mchezo huu ambao Tanzania anaingia akiwa hana cha kupoteza akihitajika kupata ushindi ili aweze kufuzu hatua inayofuata ya 16 bora katika michuano hii ambayo ni mara ya 3 kwa Taifa Stars kufuzu.

Bila shaka wengi wanaamini kuwa endapo hii leo wachezaji wa Taifa Stars wataongeza nguvu zaidi ya ile ambayo waliionesha kwa Zambia basi wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri mbele ya timu ya Taifa ya DR Congo ambayo imesheheni wachezaji wakubwa kutoka ligi kubwa barani Ulaya.

Unajua nasema kwanini Stars wanaingia katika vita ya kujuana dhidi ya DR Congo? Kumekua na wachezaji kadhaa ambao wanacheza na ambao waliwahi kucheza ambao wanaweza kutumika kutoa siri ya jinsi ya baadhi ya wachezaji wanavyocheza. Tutazame vita hii ya kujuana katika namna hii

Mwamnyeto&Bacca dhidi ya Mayele

Hawa ni wachezajia ambao wanafamiana vya kutosha kwani wameshacheza Pamoja mara nyingi katika kikosi cha Yanga kabla ya Mayele kuuzwa katika klabu ya Pyramid nchini Misri. Katika kikosi cha Tanzania,Mwamnyeto na Bacca ndio mabeki wa kati ambao wamecheza dakika 180 kwenye mechi mbili za Afcon katika michuano ya mwaka huu wakiruhusu mabao manne na straika wa Pyramids, Fiston Mayele yeye amecheza dakika 39 pekee.

Mayele kama ataanza katika mechi hii basi mabeki wa Stars wanapaswa kumchunga nyota huyo wa zamani wa Yanga kwani anawafahamu vizuri akiwa amewahi kucheza Tanzania kwa misimu miwili mfululizo.

Feitoto&Kibu dhidi ya Inonga

Hapa wanakutana wachezaji wa klabu ya Simba yaani Kibu na Inonga Pamoja na mchezaji wa Azam ambaye waliwahi kukutana katika baadhi ya mechi za ligi kuu Tanzania Bara. Kama wote watacheza mechi hiyo huenda ikashuhudiwa vita kutokana na kujuana vyema kwenye Ligi Kuu.

SOMA ZAIDI: Mauritania Na Simulizi Yao Mpaka Kumtoa Algeria AFCON

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Huyu Ndio Beki Katili Wa Nyavu AFCON - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version