Klabu ya soka ya Yanga wanatarajia kushuka Dimbani, Machi 30, 2024 kumenyana na miamba ya soka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya CAFCL utakaopigwa katika Dimba la Mkapa majira ya saa 3:00 usiku.

Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns ni mechi ambayo itakutanisha mabingwa kutoka katika nchi zao yaani Tanzania na Afrika Kusini.

Moja ya ubora wa Mamelodi Sundowns ni eneo la ulinzi ambapo katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) wamefunga mabao 33, wamefungwa goli 5 pekee katika mechi 18 huku wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Wameshinda michezo 14 (asilimia 77.78) na sare 4 (asilimia 22.22), na katika michezo yao mitano ya mwisho ya Ligi wameshinda mechi 2 na sare 3.

Kwenye CAFCL hatua ya makundi, kwenye mechi 6 walizocheza, Mamelodi wamefunga mabao 7 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja tu tena ugenini dhidi ya Mazembe.

Upande wa Yanga SC kwenye Ligi Kuu ya NBC wao wamefunga mabao 49, wameruhusu mabao 9 katika mechi 20 za Ligi Kuu ya NBC. Yanga wameshinda mechi 17 (asilimia 85), wamefungwa mechi 2 (asilimia 10) na sare mechi 1 (asilimia 5).

Katika michezo mitano ya mwisho ya Ligi, Yanga wameshinda mechi 4 na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC.

Yanga wamefunga mabao 9 kwenye hatua ya makundi ya CAFCL msimu huu na kuruhusu kufungwa mabao 6 katika michezo 6.

Kwa takwimu hizi unaona wazi kwamba Yanga wana kazi ngumu ya kupenya safi ya ulinzi ya Mamelodi katika michezo ya Robo fainali ya CAFCL.

Wafungaji, Mamelodi wana mchezaji mmoja hatari raia wa Brazil anayeitwa Lucas Ribeiro Costa (25). Kitakwimu, Costa ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji au second striker (namba 10), katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu huu wa 2023/24

Costa amecheza mechi 13, amefunga mabao 10 na kutoa assists 2 na ndiye kinara wa upachikaji mabao kunako Ligi Kuu ya PSL nchini Afrika Kusini mpaka sasa.

Kwa Yanga wao wanaye kiungo mshambuliaji, Aziz KI ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 13 na assist 7.

Kwenye CAFCL, kwa timu hizi mbili mwenye mabao mengi ni Pacome Zouzoua wa Yanga (mabao 3 na assist 1), Mudathir Yahya wa Yanga (mabao mawili na asist 1), Peter Shalulile wa Mamelodi (mabao 2 na assist 1.

Wafungaji wengine Wananchi na Mamelodi wote wana bao moja kila mchezaji.

Yanga ni;

Stephane Aziz Ki

Joseph Guede Gnadou

Kennedy Musonda

Bakari Nondo Mwamnyeto

Mamelodi ni;

Lucas Ribeiro

Teboho Mokoena

Gomolemo Grant Kekana

Thembinkosi Lorch.

SOMA ZAIDI; Kwanini Yanga vs Mamelodi Na Sio Simba vs Al Ahly?

1 Comment

  1. Pingback: Simba Ana Nafasi Ya Kuendeleza Ubabe Dhidi Ya Ahly Kwa Mkapa - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version