Ni rasmi sasa michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) kwa mwaka huu imekamilika rasmi na mwenyeji akifanikiwa kuuchukua ubingwa na kuubakisha katika ardhi yake ya nyumbani.

Achilia mbali matokeo ya kushangaza lakini pia na safari ngumu aliyoipata bingwa wa michuano ya AFCON kwa msimu huu ambaye ni mwenyeji Ivory Coast kuna mambo mengi ambayo yamejificha nyuma ya pazia ambayo unaweza kuwa huyafahamu lakini sisi tumekuandalia kwa kina kabisa mambo hayo ili uweze kuyafahamu vizuri kabisa.

  • Kwa mara ya 12 katika historia ya michuano ya mataifa barani Afrika, nchi mwenyeji anachukua ubingwa ambapo mara ya kwanza ilikua Misri mwaka 2006 huku Ivory Coast hili likiwa ni taji lao la 3 baada ya kuchukua mwaka 1992 nchini Senegal na mwaka 2015 nchini Equatorial Guinea.
  • Hii ni mara ya 5 kwa Nigeria kufungwa katika michuano ya AFCON ambapo ilitokea pia mwaka 1984,1988,1990 na mwaka 2000 wakiungana na timu ya taifa ya Ghana kama timu ambayo imefika fainali nyingi za AFCON.
  • Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast Emerse Fae, anakua kocha wa kwanza kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa wa AFCON bila ya kuanza michuano kama kocha mkuu.
  • Katika mchezo wa fainali, Nigeria amepiga mashuti pekee yaliyolenga goli ikiwa ni mashuti machache zaidi kwao tangu kuanza kwa michuano ya msimu huu.
  • Kapteni na beki wa kati wa Nigeria ameweka rekodi ya kuwa beki wa kwanza wa kati kufunga mabao 3 katika michuano ya AFCON.
  • Ekong wa Nigeria na Haller wa Ivory Coast ni wachezaji wa kwanza kufunga magoli katika mechi za nusu fainali na mechi ya fainali katika michuano ya AFCON tangu afanye Gedo mwaka 2010 nchini Misri.
  • Simon Adingra anaingia katika rekodi za CAF kwa kuwa mchezaji aliytoa pasi mbili za usaidizi katika fainali za michuano hii kwa karne ya 21.
  • Max-Alain Gradel ndio mchezaji mkongwe zaidi kushiriki fainali ya AFCON ambapo amecheza fainali akiwa na miaka 36 na siku 73 tangu itokee kwa Essam El Hadary aliekua na miaka 37 mwaka 2010 na miaka 44 mwaka 2017.

SOMA ZAIDI: Washindi wa tuzo za AFCON vipengele vyote

2 Comments

  1. Pingback: Haller Kutoka Kupambana Na Saratani Mpaka Bingwa AFCON - Kijiweni

  2. Pingback: Ratiba Kamili Ligi Ya Mabingwa Afrika Mwezi Huu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version