Ni rasmi kuwa sasa Taifa Stars imeaga michuano ya mataifa barani Afrika baada ya kumaliza katika kundi wakiwa nafasi ya 4 na alama 2 pekee kwani wamefungwa mchezo mmoja dhidi ya Morocco na kupata sare katika michezo 2 ambao ni dhidi ya Zambia na wa mwisho dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Ukiitazama namna ambavyo Taifa Stars ilivyocheza katika baadhi ya mechi za katika michuano hii utagundua kuwa kama timu ilikosa kujiamini yaani walipoteza kabisa ile hali ya kuwa na Imani na ujasiri kuwa wanaweza kufanya kitu bila kusita au kuwa na shaka yoyote ile.

Kuanzia katika maamuzi ambayo makocha wa timu ya Taifa yalikua yakionesha wazi kuwa hawakua na ile ari ya kujiamini katika baadhi ya mambo waliyokua ya msingi kabisa japokua tunafamu namna ilivyo ngumu kwa kazi ya kuusoma mchezo kwa makocha n ani moja kati ya mambo ambayo hayapingiki ndio maana baadhi ya vilabu vikubwa vinaajiri wasoma mchezo kwa ajili ya kutathmini na kutoa mapendekezo zaidi.

Nadhani ni wakati sasa wa kuwa na imani ya kwamba hatupaswi kuwaacha makocha hasa wale wa kigeni kufanya maamuzi makubwa bila usimamizi mkubwa na wa karibu bila ya kuwa na wakufunzi ambao ni wabobezi wa kitanzania kwani watajifunza kitu.

Unajua katika nchi yetu kuna wakufunzi wengi sana wa kiufundi na tunafahamu kuwa baada ya AFCON ya Morocco inayofuata ni ya kwetu tujipange mapema kabisa na tusione ubaya katika kujifunza. Kwa Tanzania, AFCON ndo Kombe la Dunia na CHAN ni AFCON kwetu na tulimpa kocha mamlaka makubwa mno, tukaacha kujiamini leo tunalalamika.

Katika mchezo dhidi ya DR Congo ilikuwa mechi yetu ya kufa au kupona, kwahiyo tulipaswa kuwa na mpango wa kushambulia kuliko mpango wa kupasıana sana kuelekea langoni kwetu, walimu wana imani yao. Nina imani pia kwamba pamoja na mpango wetu mzuri wa kujilinda ila tulipaswa kuwa na mpango mzuri pia wa kushambulia na kuwa na wachezaji wenye asili ya kushambulia zaidi wa kufanya hilo. Namna tulivyocheza haikuakisi sana kwamba tunataka kuvuka na tuna mpango mzuri wa kushambulia. Siamini kwamba hatukuwa na wachezaji hao ila hatukuwa na mpango huo, mabadiliko yalivyofanyika yanaakisi imani yangu.

SOMA ZAIDI: Huyu Ndio Beki Katili Wa Nyavu AFCON

1 Comment

  1. Pingback: Ratiba Kamili Ya AFCON Hatua Ya 16 Bora - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version