Ni fahari kubwa kwa ulimwengu wa sasa kujivunia nafasi kubwa ya wanawake kwenye jamii yetu jukumu mama la malezi limefanywa kwa ubora na muendelezo kila siku, nafasi yao ni kubwa kwenye jamii. Nje ya malezi na usimamizi wa familia ila Dunia ya sasa imempa nafasi ya kufanya vitu mbalimbali kusoma na kuwa na ujuzi wa hali ya juu kupata nafasi za juu za uongozi na mambo mengine mengi ya kijamii.

Lakini kurasa ya leo imefunuliwa kivingine kwenye upande wa pili wa maisha nje ya hayo na kunikumbusha baadhi ya majina kichwani mwangu Sophia Mwakisili, Edna Lema na Ester Chaburuma.

Ilikuwa siyo rahisi kwao kujihusisha na upande huu wa kusakata kabumbu, ilikuwa ngumu kuanzia kwao na hata jamii pia kushindwa kukubaliana na ilo, ilikuwa ngumu kwa familia kukubali kumruhusu mtoto wa kike kujihusisha na soka au kabumbu ila kwa sasa mapinduzi hayo yamefanyika

Soka la wanawake kwetu sisi tulikuwa tukishuhudia kwa wenzetu kupitia runinga au televisheni ila kwa sasa imeanza kuzoeleka baada ya kushuhudia mabadiliko hayo, wanadada wengi wameboresha maisha yao kwenye mpira wa miguu na kuonekana sehemu kubwa ya wapenda mpira hususa kwenye bara la Afrika na nje.

Ligi kuu ya Wanawake maarufu kama Serengeti Women Premier League ina zaidi ya miaka mitano sasa imeleta mapinduzi makubwa ya Mafanikio kwenye upande wa mpira wa miguu, kupitia Serengeti Women Premier League wachezaji wengi wa Kitanzania wamepata nafasi ya kuonekana ndani na nje ya Tanzania. Kumbukizi bora imembeba Sophia Mwakisili akiwa ni msakata kabumbu wa kwanza wa Kike kucheza soka la kulipwa nje ya bara la Afrika ndani ya klabu ya Luleburzag Ya Uturuki akiwa ni Nahodha wa Twiga Stars na alijiunga na Luleburzag akitokea Simba Queens ila kwa sasa ni sehemu ya Benchi la ufundi la Simba Queens akiwa kama Meneja wa timu.

Soka la wanawake kwa sasa limekuwa na wachezaji wengi wamepata “Plattform” kuonyesha uwezo wao na wengi wao ni wachezaji wadogo na wenye uwezo. Historia ya Ligi kuu ya wanawake imeshuhudia mabingwa mara saba huku ikiwa ni vilabu viwili tu vikichukua  ubingwa huo ambao ni Simba queens na JKT Tanzania ambao ndiyo vilabu vilivyotawala soka ilo kwa muda mrefu sasa, JKT Tanzania akiwa na ubingwa huo mara 4 akifatiwa na Simba queens mara matatu. Miaka mitano nyuma Ligi kuu ya Wanawake ilitawaliwa na Simba queens pamoja na JKT Tanzania ila kwa sasa inaushindani kutoka kwa vilabu vingine kama Yanga Princess, Fountain Princess na Ceasian Queens.

Ndani ya miaka saba ya kukua kwa Soka la Wanawake tumeshuhudia mabadiliko na mafanikio makubwa sana, kupitia Soka la wanawake wachezaji wengi wazawa wamefanikiwa kutoka nje ya nchi kwa kucheza soka la kulipwa na hata kuongezeka kwa makocha wa kike kwenye timu za Ligi ikiwemo Edna Lema maarufu “Mourinho” akiwa ni Kocha msaidizi wa Biashara United na timu ya vijana ya wanawake huku akiwa ni kocha wa zamani wa Yanga Princess, Sophia Mwakisili ambaye ni Meneja wa Simba Queens na mchezaji wa zamani wa Twiga stars, pamoja na Ester Chaburuma ambaye ni Kocha mkuu wa JKT queens.

Mpaka sasa wachezaji wa kike wapatao nane (8) wanacheza soka la kulipwa nje ya bara la Afrika ambao ni mshambuliaji Clara Luvanga ambaye anacheza Al Nasri ya Saudi Arabia akiwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga Princess, Opah Celent anayekipiga Besiktas ya Uturuki akitokea Simba Queens, Aisha Masaka akikipiga BK Hacken akitokea Yanga Princess, Maimuna Hamis akiichezea Zed FC akitokea Simba queens, Julitha Singano akicheza Juarez FC akitokea Simba Queens pamoja na Enekia Lunyamila akikipiga Eastern Flames ya Saudi Arabia.

Uwepo huo wa wachezaji wengi hao wakicheza soka la kulipwa ni sehemu ya upigaji hatua kwa Soka la wanawake, nje ya wachezajibhao wanokipiga nje ya nchi ila tumeshuhudia wachezaji wengi wanaokipiga ndani wakiwa na viwango bora kama Stumai Abdallah wa JKT Tanzania, Winfrida Gerrard, Najiath Idrisa, Fatuma Issa, Donisia, Irene Kisisa na wengine wengi wakisakata kabumbu ndani ya nchi.

Ukuaji huo umeshuhudia vilabu viwili vya Ligi ya Wanawake kutokea Tanzania vikishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake mara mbili mfululizo ambapo mwaka 2022 Simba SC alishiriki na kuishia hatua ya Nusu Fainali na mwaka 2023 ilishuhudia JKT Tanzania ikishiriki tena na kuishia hatua ya Makundi hiyo ni moja ya hatua iliyopigwa kwenye upande wa Wanawake

Soka ilo limeleta mafanikio makubwa kwenye upande wa timu za taifa na kupitia soka la wanawake imeshiriki michuano ambayo timu za wanawaume hawajawahi kushiriki ikiwemo kuchukua Kombe la COSAFA pamoja na kushiriki michuano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 17 maarufu kama “U-17 World Cup” ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa timu ya taifa yoyote nchini kushiriki michuano hiyo.

Familia na wazazi wengi walikuwa wakiwanyima nafasi vijana wao wa kike kwa kuona mpira wa miguu kwa mwanamke unamfanya kuishi kwenye maisha au “kuwa na pigo za kiume” kitu ambacho ni tofauti kabisa kwani wapo baadhi ya wachezaji wa kike wanacheza huku wakiwa wamefunika mwili mzima au kufunika kichwa kulingana na dini yake na mfano mzuri kwa hapa kwetu ni beki wa Simba queens Fatuma Issa “Fetty densa” na kuibadilisha jamii kwenye ilo.

Wanawake wanasifika kuwa na usimamizi pamoja na upangaji wa mambo na ilo limedhihirika kwa wachezaji kufungua maduka na biashara mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwaingizia hela kama Opa Clement akimiliki biashara ya kuuza Juice “Opa Juice” na kuwezesha kuwakomboa vijana wengine kwa kuwapa fursa na kuingiza kipato pia kuna Fatuma Issa na hiyo inaelezea maana halisi ya ukimpa nafasi mwanamke basi atarudi na kushukuru.

Familia nyingi za baadhi ya wacheza kabumbu wa kike zimebadilisha maisha yao kutokana na kuwaruhusu watoto wao wa kike wenye kipaji kusakata kabumbu. Mpira wa miguu ni pesa na moja ya njia ya kupiga pesa ni kuanza nyumbani kupata nafasi ya kwenda nje ya nchi ambapo kuna malipo mazuri kama ambavyo Opa Clement, Aisha Masaka, Clara Luvanga na wengine wengi.

Jamii iendelee kuwapa nafasi na imani yangu kubwa ni kuwa baada ya miaka mitano hadi saba mbele soka la wanawake litakuwa moja ya chanzo cha mapato kwa familia na wachezaji wenyewe.

SOMA ZAIDI: Dube Unapoelekea Unakosea Ungekaa Kimya Tu Kwanza

Leave A Reply


Exit mobile version