Skudu Makudubela ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapata wakati mgumu kupenya kwenye Kikosi cha kwanza cha Miguel Angel Gamondi kwa sababu kocha huyu ukimtazama lakini pia ukiitazama timu inavyocheza ni muumini wa mchezaji ambaye ana faida wakati timu yake ikiwa haina mpira mguuni na ndio maana wananchi wanavyocheza wanakua nit imu ambayo inakua na kasi sna wnapokua kwenye upande wa mpinzani.

Gamondi ni kocha ambaye anataka mchezaji ushiriki katika kusaka mpira kwa kasi sana pindi tuu ukipotea kwenye himaya yenu, jambo kubwa unalotakiwa kufanya ni kuanza kumnyima mpinzani wako nafasi ya kupitisha mpira ukiwa kwenye himaya yake nah ii ndio faida kubwa waliyonayo Yanga hivi sasa kwakua wanakua haraka sana kuupambania na kuurejesha mpira katika himaya yao pale tu ukipote miguuni mwao.

Skudu ni mchezaji ambaye jinsi anavyocheza uwanjani hawezi kufanya kazi hiyo kwa sababu yeye ana furahia  zaidi kucheza Soka kwa kuuchezea mpira ukiwa katika himaya yake na ukimpotea basi anakua hana uwezo wa kuutafuta kwani ni mvivu kwenye kukaba.

Nyota huyu amekosa nafasi ya kucheza Yanga kwa sababu za ki mfumo tuu lakini si kiwango chake kidogo, yule Maxi Nzengeli, Augustine Okrah na nyota wengine wote wanaocheza pembeni pale Yanga Wana faida hata timu yao ikipoteza umiliki wa mpira kwani huwa wanakaba na wana kasi.

SOMA ZAIDI: Itawachukua Muda Mrefu Sana Yanga Kumpata Golikipa Mwingine

1 Comment

  1. Pingback: Yanga Ya Gamondi Inamchanganyia Mafaili Benchikha ? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version