Sitorudi nyuma kuandika ukweli japokua ni jipu chungu kwenye mioyo ya wanasimba ambao bila shaka wengi wamekua wakipumbazwa na propaganda za takwimu kuhusu Simba na wachezaje wake wakati wengine wakiendele kubadilika na kukua kisoka.Ukweli mtupu huu Kama utafanyiwa kazi basi utaleta furaha na kukata kiu ya mtu alietoka jangwani baada ya kupigwa jua kali.

Mpaka sasa Simba kwa misimu miwili hii ina makombe mawili tu kabatini yaani kombe la MAPINDUZI na NGAO YA JAMII na ukipiga tathimin hayo makombe siyo lolote siyo chochote lakini kubwa zaidi imeleta kocha mpya (BENCHKHA) lakini swali la kujiuliza je Simba sc wanabadili makocha je wao pia wanaweza kusajili wachezaji wenye hadhi kama makocha wanavyotaka?

Jibu ni hapana! Ukiangalia kuletwa kwa kocha Robertinho hakuna wachezaji wazuri walioletwa ili kwenda na Falsafa za kocha Robertinho Ila tu kilichofanyika ni ujanja ujanja na kununua wachezaji wa mafungu (Bei Chee).

Nikuulize tu swali, nani aliyemleta Sawadogo, Nelson Okwa na wachezaji wengine walioonekana kabisa hawana hadhi ya kucheza Simba sc? Hapo tunapata picha kuwa Kocha anapendekeza mchezaji huyu lakini viongozi (wazee wa ten percent) wanaleta wachezaji wanao wataka wao.

Ameletwa kocha mpya BENCHKHA kwa takwimu ni kocha mzuri lakini ukija kwenye timu aliyopewa hakuna wachezaji wazuri na timu ikifanya vibaya lazima atafukuzwa tu na atatafutwa kocha mwengine.

Nadhani niwaambie wazi tu kuwa nafungua ubongo wa msomaji kuwa mchele ni ngumu kupikwa na chuya Ina maana ujio wa kocha mpya akikabidhiwa timu yenye wachezaji Kama Saidoo Ntibazonkiza, John Bocco, Chama n.k Basi itakua ni kazi ya kutwanga maji kwenye kinu n ani wakati sasa wa Simba sc kuondoa wazee katika kikosi hata aje Mourinho au Guardiola nao watafukuzwa tu baada ya mechi.

SOMA ZAIDI: Dube Unapoelekea Unakosea Ungekaa Kimya Tu

1 Comment

  1. Pingback: Ni Wakati Wake Sishangai Haya Mapambio Kumhusu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version