Ni takribani miaka kumi na tano sasa tokea kuanza kushuhudia Tamasha la klabu hapa nchini, ni dhahiri kuwa aliyebeba na kubuni wazo ilo anahitaji pongezi kubwa sana na watoto wa mjini wanasema kuwa ana mahala pake mbinguni au tuseme kuwa apewe maua yake, yote hayo ni maneno juu yake.

Ilikuwa ngumu kuamini kama itakuja kuwa moja ya tukio kubwa na bora sana kwa vilabu hapa nchini na nje ya nchi, mwanzoni iliwekwa kwenye uzani wa kiutani zaidi na hata ilikuwa ngumu kukubalika na kuigwa na wengine.

Sasa imekuwa kitu muhimu sana imekuwa ikiwaleta na kuwaweka pamoja mashabiki, wapenzi wa Soka na wafuatiliaji wote wa mpira nchini kwa ajili ya msimu mpya wa Mashindano kwa vilabu vyao.

Imekuwa burudani, imekuwa sehemu ambayo watu wa mpira wakifurahi kwa pamoja, imekuwa sehemu ya kurudisha kwa jamii, nje ya kuangalia burudani ya Soka ila na jamii nayo inanufaika nayo.

Kwa takribani miaka mitano ya hivi karibuni vilabu vingi sana vimeanza kuiga utamaduni ambao ulikuwa unafanywa na Simba SC pekee, mpaka kufikia mwaka 2017 ilikuwa ni klabu pekee yenye Tamasha Lao kwa ajili ya kutambulisha kikosi kazi cha msimu mpya wa Mashindano, lakini mpaka kufikia 2024 ni zaidi ya vilabu vinne navyo vinafanya.

Alianza Yanga SC akiita Wiki ya Mwananchi, akafuata Azam FC naye akilipa Jina la Azamka, msimu huu ni vilabu vya Simba SC, Yanga SC, Pamba Jiji FC wakiita Jina la Pamba Day, Mashujaa wakiipa Jina la Mashujaa Day pamoja na Singida Blacks Stars ambayo yao inajulikana kama Big Day.

Jambo ambalo ni zuri ni kuwa mwanzoni tulizoea kuiona inafanyika Dar es Salaam tu ila kwa sasa hadi kwa vilabu ambavyo vipo nje ya Jiji ilo, msimu huu utambulisho wa Vikosi vya timu tano utafinyika kwenye mikoa minne tofauti Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma pamoja na Singida.

 

Tukio ilo limeenda mbali sana kwani hata vilabu kutoka nchi jirani navyo vimeanza kufanya kama ambavyo nyumbani wanafanya, na hiyo haijaja tu Bali ni baada ya kuwa wakialikwa kuja kucheza kwenye siku hizo, namna tukio yanavyokuwa yanaendeshwa yamewavuti sana, tumeona APR amewahi kufanya hivyo pamoja na Rayon Sports zote za Rwanda nazo zimeweka siku yao ikiwa ni baada ya Mara kadhaa kuja kucheza nchini.

Pongezi kubwa sana kwa muhasisi au muanzilishi pamoja na jopo zima lililokuja na wazo ili na kuamua kulitekeleza huku kukiwa na muendelezo kwani siyo rahisi kuanzisha jambo na kuwa na muendelezo nalo.

Nje ya hilo kwa sasa imekuwa ni vita ya namna ya kufanya tukio ilo kuwa kubwa na la kuvutia kuliko mwingine, imefikia hatua namna ya kufanya tukio ilo kufana basi mashabiki kupata ubunifu mkubwa kuanzia mitandaoni mpaka uwanjani.

SOMA ZAIDI: Hiki Ndio Kipindi Ambacho Afrika Inaiogopa Simba Na Yanga

7 Comments

  1. Sio kweli kwamba simba walianzisha bali na wao waliiga kwa majirani zetu ndipo yeye akawa na rekodi kubwa

  2. Kossam beneth on

    Jambo ni jema na ndiyo maana hata wengine wameamua kuiga na kufanya
    Pongezi kwa mwasisi na simba kwa ujumla
    Ubaya ubwela

  3. Pingback: Barua Kwenu Washambuliaji Kuelekea Msimu Wa 2024/2025

Leave A Reply


Exit mobile version