Kama Taifa tumeshajipanga kuwa na Chama au Pacome, lazima tuwe wajanja katika hili hatupaswi kuendelea kuwasifia wachezaji wa mataifa ya wenzetu wakati sisi timu yetu inakwama.

Leo tunamshangilia Clatous Chama, Pacome Zouazoua anaimbwa sana lakini kupitia wao tuandae mpango mzuri wa kesho na sisi kuwa na wachezaji wa namna hii.

Wanasema, siyo vibaya kuiga kitu kizuri hata kidogo tuwatazamapo hawa lazima tuwe na kawivu kidogo kwani hatutaki kuwa na wachezaji wa namna hii, ni nini kilifanyika pale Zambia wakampata Chama, Ivory Coast na Asec yao hua wanafanyaje wanakuwa na wachezaji wa aina hii, naamini hatujashindwa sisi.

Tusikalie kila siku kuwashindanisha nani mbora zaidi ya mwingine na kusahau la msingi. Hawa soka lao lipo mbali wametuacha kilometers nyingi lakini tusikubali watuachie vumbi, tuibe nini wakifanyacho hawa ili tuwe na wakina Pacome wetu.

Tunawasahau sana wachezaji wetu wa ndani ambao mara nyingi huwa ndio haohao tunawategemea kwenye timu yetu ya taifa yaani Taifa Stars, ni wazi kuwa tunawashindanisha na kuwakuza wachezaji wa timu za taifa zingine kabisa na kuwapa majina makubwa kulingana na kile ambacho wamekua wakikionesha ukweli ni kuwa wote wana vipaji vikubwa sana.

Mjadala unaowahusiha wachezaji hawa una wafaidisha zaidi wao wenyewe na adala yake nadhani ni muhimu kuwapambanisha wachezaji wetu wa ndani ili kuhakikisha kuwa wanajituma zaidi na kuipambania nchi yetu na kuvipambania vipaji vyao.

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga

Leave A Reply


Exit mobile version