Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate imetangaza rasmi kuhamia katika uwanja wa Black Rhino Academy uliopo wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Kupitia kwa mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano wa klabu hiyo Hussein Masanza amesema kuwa uamuzi huo unakuja baada ya uwanja wao wa nyumbani wa CCM Liti kufungiwa na bodi ya ligi ili kupisha marekebisho.

Kikosi cha klabu ya Singida Fountain Gate wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi ambayo wamecheza katika uwanja wa CCM Liti Singida.

Aidha kupitia taarifa hiyo ambayo wamechapisha katika kurasa zao za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, Masanza anasema kuwa watautumia uwanja wa Black Rhino Academy hadi pale ambapo uwanja wa CCM Liti uliopo Singida utakapokamilika.

Klabu ya Singida inatarajiwa kucheza mechi mbili katika uwanja wa akademi ya Black Rhino ambapo watacheza disemba 11 dhidi ya KMC ambao utakua mchezo wa ligi kuu lakini pia disemba 15-17 dhidi ya Arusha City mchezo wa kombe la shirikisho la Azam .

Fuatilia uchambuzi wa Amri Kiemba hapa Pacome na Chama Nani Bora?

 

Leave A Reply


Exit mobile version