Simba Wana Jambo lao..! Kiungo mshambuliaji wa Singida, raia wa Brazil Bruno Gomes ameitwa jijini  Dar es Salaam  kwa ajili ya kumalizana na mabosi hao wa Msimbazi kabla ya kutangazwa kuwa mmoja ya nyota wapya wa timu hiyo kwa msimu ujao ambao Wekundu wamepania kurejesha heshima.

Tayari Bruno aliyefunga mabao 10 msimu huu kwenye ligi, yuko Dar es Salaam akiambatana na viongozi wa Singida na kama mambo yataenda kama ilivyopangwa atasaini mkataba wa miaka miwili.

Mbrazili huyo pia ni pendekezo la Robertinho ambaye aliwaambia vigogo wa Simba anamtaka ili akasaidiane na Clatous Chama, Saidi Ntibazonkiza na Mzamiru Yassin eneo la kiungo.

Moja ya vigogo wa Simba alithibitisha  nakusema “Onana na Gomes ni shabaha yetu na kuanzia kesho mnaweza kuona tarifa rasmi kuhusu wao,” alisema kigogo huyo na kufafanua;

“Tayari huyo winga (Onana) tumemalizana naye na sasa tupo kwenye hatua za mwisho kumsainisha Bruno kwani tupo naye hapa Dar es Salaam, ikiwa ni mwanzo wa pazia la usajili kwa kikosi kijasho.”

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alithibtisha timu yake msimu huu itachukua mchezaji inayemtaka kwenye timu yoyote.

“Siwezi kuweka wazi tumemsajili nani na nani lakini unachotakiwa kujua ni kwamba kila mchezaji tunayemtaka tutampata bila shida yeyote. Simba ni timu kubwa,” alisema Ahmed.

Kwa taarifa zaidi za michezo, tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version