Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3:0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliofanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam.

Mchezo huo uliokua wa kuvutia ulimalizika kwa kipindi cha kwanza klabu ya Simba kuondoka na ushindi wa bao 1:0 lililofungwa na kiungo wake Saido Ntibazonkiza kwa njia ya mkwaju wa penati.

Dakika ya 75 wekundu wa msimbazi waliongeza uongozi kwa bao safi la kichwa lilofungwa na kiungo mmali Sadio Kanoute huku Mshambuliaji na kapteni wa klabu hiyo John Raphael Bocco akishindilia msumari wa moto kwa kufunga bao la 3 dakika ya 90 ya mchezo.

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi tisa na wote wapo nyuma ya Azam FC yenye pointi 28 za mechi 12.
Kwa upande wa Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 13 za mechi 12 nafasi ya 12.

Aidha baada ya mchezo huo kocha mkuu wa klabu ya Simba, Abdelhak Benchikha ameweza kuwasifu wachezaji wake kwa ushindi walioupata lakini akilia na ubovu wa sehemu ya kuchezea wa Uwanja wa Uhuru huku kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime akisema kuwa wanaendelea kujipanga kuhakika wanarekebisha makosa ya leo na kushinda mchezo unaofuata.

Kwenye msimamo anaeongoza ni Azam Fc akiwa na alama 28 na mechi 12 alizocheza huku anayemfuatia ni Yanga ambae amecheza michezo 9 na alama 24 huku wa tatu ni klabu ya Simba ambae amejikusanyia alama 22 katika mechi 9 alizocheza.

Klabu za Geita Gold , Mashujaa na Mtibwa Sugar zikiwa chini kabisa ya msimamo wa ligi kuu Tanania Bara.

Kwa taarifa zaidi za michezo unaweza kuendelea kwa kusoma hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version