Mchezo mzima ukiutazama wa ligi kuu hii leo ni wazi tu kwamba kuanzia kipindi cha kwanza ulikua ni wa upande mmoja huku Simba wakitaka kutuma salamu kwa wapinzani wao wanaoenda kukutana nao katika ile mechi kali ya Mzizima kati yao na matajiri wa Chamazi klabu ya Azam.

Kuanzia kipindi cha kwanza ambacho kwa asilimia kubwa klabu ya Simba waliumiliki zaidi mchezo huku kikosi cha Tabora kukutana na upinzani mkubwa zaidi katika dimba la Ali Hassan Mwinyi kwani hawakua wakicheza kama timu kwa pamoja zaidi sana ilikua uwezo wa mchezaji mmoja mmoja huku wana lunyasi wakiwa na uwezo wa kufunga zaidi ya mabao waliyopata lakini kubwa zaidi katika ligi ni alama 3.

Ukiwatazama Tabora walicheza wazi sana kitu ambacho ni hatari unapocheza na timu kubwa hawakuwa na kasi na ile ari ya kutaka kupata angalau sare dhidi ya wekundu wa msimbazi  kuanzia eneo la kuzuia, kutengeneza na kumalizia. Hawajulikana au hawajui wapi wanapaswa kuchezaje walau kuwapa presha Simba.

Simba wamekuwa huru sana na mpira kuanzia wanapozuia wanapata presha ndogo kwani Tabora hawakuwa wakifanya pressing kuanzia juu lakini pia hawachezi kwa kujilinda kwa tahadhari kubwa kwamba wamepaki basi kwani walikua wazi sana jambo ambalo walifanya kikosi cha Simba kufurahia zaidi na kushinda kiasi hicho cha mabao.

Kwanza mabao mawili ya Simba ya kipindi cha kwanza unaona kabisa waliofunga walikua hata hawajabughudhiwa na kufunga free header unajiuliza mtu anafunga bila kughasiwa ndani ya 18 ya wapinzani. Kama Tabora hawatobadilika watapokea kipigo kikubwa kutoka kwa baadhi ya timu ambazo zina matumizi mazuri ya mipira ya juu.

Chama ameendelea kuwaonesha mashabiki na viongozi wa simba kwamba yeye ni kiungo bora sana nah ana mpinzani katika ligi hii kwa ubora ambao ameuonesha hii leo lakini hili ni wazi kuwa mashabiki wafahamu kuwa kipimo cha Tabora sio kipimo ambacho atakutana nacho mbele ya Azam wanatakiwa kuongeza umakini na kucheza vizuri zaidi nah ii ni wazi Simba wanaonyesha hasira kuelekea MZIZIMA DERBY Ijumaa inayopigwa Mwanza.

SOMA ZAIDI: Ligi Kuu Imerejea Marefa Kuweni Na Msimamo

1 Comment

  1. Pingback: Yanga Dhidi Ya Mashujaa Tusitarajie Mechi Ngumu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version