Nikiri kuwa sipingani na jambo hili lakini ni wazi kuwa uongozi wa klabu ya Simba unapaswa kuwa makini zaidi kwani ndio eneo ambalo mara nyingi mashabiki hufurahia wakati wakitambulishwa wachezaji lakini wakiwa uwanjani mambo hubadilika kwao n ani wachache sana ambao huja na kuingia katika kikosi moja kwa moja.

Ni wazi kuwa katika kikosi cha klabu ya Simba yule Skauti amefanya kazi kubwa tu ya kuleta wachezaji wapya na wazuri na naelewa kuwa skauti kazi yao ni kufikisha kwa benchi la ufundi ambapo ndio wanafanya kazi yao ila mchezaji kuwa productive kwenye kikosi ni jambo lingine,

Kufanya scouting ni jambo moja na mchezaji kuingia katika kikosi cha kwenye timu ni jambo linguine kwani Simba tatizo lake sio ufungaji tu angalia hata eneo lake la ulinzi, angalia kiungo mkabaji anacheza kama namba 8 na namba 8 sijui atacheza kama nani?, Naweza sema kuwa simlaumu skauti wa Simba kisa timu haifanyi vizuri, hata wakina Baleke walikuwa wanakosa magoli ya wazi.

Mels Daalder ndiye mkuu wa skauti kwa wekundu wa msimbazi lakini sio anachokifanya ni bora hata mngewachukua wachambuzi wetu kama akina Shafii Dauda tujue hata akileta mchezaji nini aambiwe mapema au mashabiki wajue tu anayekula pesa za skauti Simba ni Mtanzania mwenzetu

Kina Freddy sikatai ni wachezaji wazuri ila wanahitaji kupewa muda na ukweli dirisha dogo siyo la kufanya usajili wa mchezaji kumsikilizia, unatakiwa ufanye usajili wa aina ya Ntibazokiza ambao waliingia kwenye kikosi moja kwa moja na kuanza kuisaidia team

Dirisha dogo ni la kusaka mchezaji/wachezaji wachache kwa lengo la kuongeza nguvu maeneo kadhaa tu, unakuwa na Scouting team inakuletea wachezaji wa majaribio

SOMA ZAIDI: Ni Wakati Wake Sishangai Haya Mapambio Kumhusu

1 Comment

  1. Pingback: Yanga vs Ihefu Wachezaji Hatari Wa Kutazamwa Hii Leo - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version