Ilikuwa ni vita Ya kimbinu kwa timu zote mbili Simba SC wakiingia kwa kufunguka zaidi na Tanzania Prisons pia nao wakifanya hivyo huku Simba SC wakiamua kuanzia kutoka nyuma kwenda mbele kwa pasi fupi fupi kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa Tanzania Prisons ambao wao waliamua zaidi kupiga pasi ndefu pale wanapokaribia eneo la kati.

Kipindi cha kwanza timu zote zilitengeneza nafasi kadhaa hususa Simba SC ila namna walivyokuwa wanazuia Tanzania Prisons ilitoa nafasi finyu kwa Simba SC kuwa huru eneo la lango lao na mipira mingi kuwa inapotea inatoka nje au kipa kuidaka. Simba SC wakiwa wanashambulia walikosa mtu ambaye Angekuwa anakutana na mipira yote Ya pili “Second ball” inayookolewa na Tanzania Prisons hivyo mipira mingi iliyokuwa inaokolewa ilikuwa unakutana na wachezaji wa Tanzania Prisons na wanaiondoa kwa urahisi.

Wakati wanashambuliwa Prisons waliamua kumuacha Samson Mbangula pekee yake eneo la kati la uwanja huku Zabona Hamis Mayombya akitokea pembeni upande wa kulia na Joshua Nyantini akitokea kushoto kitu ambacho kiliwafanya kumiliki mpira na kumsubiri Mussa Haji ambaye mara nyingi alikuwa akipokea mipira ya pili baada ya kuokoa na kuisambaza kushoto kulia au kupita kati kati ya uwanja kutengeneza shambulizi Mara kadhaa walikuwa wanashinda kutokana na eneo la beki wa kati la Simba SC kutotulia na kuacha nafasi “gap” kubwa baina Ya Henock Inonga na Kennedy Juma na hiyo imesababishwa na wachezaji hao kuwa wanafuata mpira na kuacha nafasi kubwa kiufupi hapakuwa na utulivu mkubwa.

Goli la kwanza la Prisons ilitokana na kushindwa kurudi mapema kwa wachezaji wa Simba SC lakini pia ni uhodari mkubwa kwao kutumia nafasi hiyo, mkimbio “movement” ya goli ilo inaonyesha kiasi gani Prisons waliisoma Simba SC ikiwa inashambulia ndiyo maana baada Ya kuondosha hatari goli kwao ilikuwa rahisi kuwashinda “kuwawin” Simba kwa kuwa na mpambano wa wachezaji wawili kwa wawili kwa timu zote Samson Mbangula na Zabona Hamis dhidi Ya Babaca Sarr na Kennedy Juma na kasi ya Mbangula Samson ilisaidia zaidi kupata goli japokuwa kuna uzembe ambao kama golikipa Aish Manula alipaswa kutoka golini kusaidia kupunguza goli na hata Mbangula aliposhindwa kukokota mpira vizuri ingekuwa rahisi kwake kuokoa kwa kuudak au kuutoa.

Kipindi cha pili ilikuwa ni vita Ya mipira mirefu kwa timu zote mbili huku Simba SC wakishambulia zaidi kutokea pembeni kuingia ndani huku Tanzania Prisons wakitumia “Caunter Attack” kupitia pembeni na pale wanapoweka mpira chini walikuwa wanajaa wengi kwenye nusu Ya Simba SC na kuwapa presha wachezaji wa Simba SC kitu ambacho kilisababisha goli la pili na Prisons walikuwa wakifurahia kuokoa “transition” za Simba na kumiliki mpira.

Baada Ya goli la pili Prisons walibadilika kiuchezaji na kubaki eneo Lao zaidi na kitendo cha kumtoa Samson Mbangula iliwapa uhuru zaidi Simba SC kutulia na mpira na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wao kukimbia kuelekea kwenye lango la Prisons na ndiyo maana walikuwa langoni mwa Prison kwa muda mrefu na mipira mingi waliyokuwa wakiokoa ilikuwa ikiangukia kwa Clatous Chama na Fabrice Ngoma, ugumu kwa wao kufunga ulikuwepo pale wakikaribia lango la Prisons wachezaji wengi walikuwa walikuwa wamejaa kwenye 18 yao ndani Ya box wakiwa watano na wengine wakiwa nje Ya box lao jambo ambalo mipira mingi waliweza kuikoa.

Mabadiliko ya Edwin Balua yalisababisha kuharibu eneo la mbele la Prison kwani muda mwingi alikuwa akicheza mbele ya goli la Prison na kumpa nafasi Chama Clatous kugawanya mipira pembeni kwa Ntibazonkiza na Ladack Chasambi wakibadilishana na Shomari Kapombe upande wa kulia na Israel Mwenda huku akisaidiana na Fabrice Ngoma kupiga krosi kutokea upande wa kushoto na wakifanikiwa zaidi kwenye ilo kilichobaki ni kuingiza mpira nyavuni tu.

Pongezi ni kwa Kocha wa Prisons Amada Ally na benchi zima kwa kuweza kuisoma vizuri Simba SC na wachezaji wao kutumia nafasi chache zilizopatikana, kiufupi Simba SC hawakuwa vizuri eneo Lao la ulinzi na makosa mengi yalikuwa yakitokea hapo na hata magoli yote ni uzembe kushindwa kunusa hatari hususa goli la pili walilofungwa.

SOMA ZAIDI: Dondoo Na Takwimu Zote Simba Dhidi Ya Tanzania Prisons

1 Comment

  1. Pingback: Azam na Simba Inawarahisishia Yanga Kuchukua Tena Ubingwa? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version