Simba wameitisha mkutano wa waandishi wa Habari nakuzungumza nao kupitia msemaji wao Ahmed Ally kuelekea mchezo wao dhidi ya Asec Mimosas pamoja na viingilio vya mchezo huo, Pia akigusia zaidi Tuzo ya mashabiki bora waliyopokea kwenye mashindamo ya AFL
Akizungumza na waandishi wa Habari Ahmed ally amesema ” “Leo tunazungumzia maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.”
“Utachezwa siku ya Novemba 25, 2023 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa Wageni watawasili Novemba 23, 2023 wakiwa na msafara wa watu 31 Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Misri.”
“Viingilio vya mchezo huu ni; Mzunguko – Tsh. 5,000, VIP C – Tsh. 10,000, VIP B – Tsh. 20,000, VIP A – Tsh. 30,000, Platinum – Tsh. 150,000.”
“Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa”
“Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.”
“Tupo katikati ya mashindano lazima tutafute kocha ambaye yupo active, atakuwa tayari kuanza majukumu ili akifika kazi ianze.”
“Kuhusu majeruhi Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha Akipona atarudi kutumikia klabu.”
“Wageni rasmi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas watakuwa ni mashabiki wa Simba Kwanza wametoka kushinda tuzo ya mashabiki bora hivyo kila Mwanasimba akija siku hiyo ajue yeye ni mgeni rasmi.”
“Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.”
“Siku hiyo tukawaonyeshe sisi ni mashabiki bora kwa kuja wengi uwanjani Lakini pia tuna wajibu wa kwenda kuipigani Simba yetu Pamoja na yote uliyonayo moyoni lakini wewe ni shabiki wa Simba, ukisusa maana yake unainunia Simba yako.”
“Wachezaji sisi tuna imani nao, tarehe 25 wakaendeleze makubwa. Waamke sasa wakaipiganie Simba. Wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa wao kufanya vizuri. Tukipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa tunayopita hivi sasa.”
“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba.”
“Tutakuwa na hamasa kama kawaida, na tutaanza mapema kuanzia Jumatatu tukiwa na matukio mbalimbali ya kuwahamasisha mashabiki kuja uwanjani Ratiba tutatoa Jumapili ya mtaa kwa mtaa. Tunataka kuujaza Uwanja wa Mkapa, tuwaonyeshe kwamba hii ni Simba.”
“Tutakuwa na jezi maalumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama mnavyojua mdhamini rasmi huwa hatumiki kwenye jezi ya mashindano hayo na kwa miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia Visit Tanzania. Kuanzia Jumatatu tutatoa taarifa itakavyokuwa msimu huu.”
“Nimepewa baraka na viongozi wa klabu kutembelea matawi ya Simba nikianza na jana katika Tawi la Simba Soko la Samaki Msasani, Tunafanya hivi kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Wanasimba. Kupokea maoni yao na kuwaalika kuja uwanjani.”
“Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL 2023 haitakaa kwenye ofisi za Simba bali itakuwa inatembea kwenye matawi mbalimbali. Lakini pia tutakuwa na mfano ya tuzo kama hii ambayo tutaipeleka sehemu mbalimbali ili wabaki na kumbukumbu”
“Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi. Wakati ujao wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena. Mwiba unatokea ulipoingilia.”
“Tiketi tunaanza kuuza leo, nunueni tiketi twendeni uwanjani. Ni kweli tulikuwa hatuchezi mpira wetu wa kuvutia lakini tunakwenda kubadilisha benchi la ufundi, tunategemea Simba itakayokuja kuwa na mabadiliko.”
“Safari hii tunakwenda kuwashangaza watu, tutaujaza uwanja wa Mkapa. Niwambie Wanasimba kama una hasira uje nazo furaha utaikuta uwanjani.”
“Kauli mbiu yetu ya mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ni Twendeni Kinyama, Mashabiki Bomba.”
Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa