Mchezo wa 18 kwa Simba SC na mchezo wa 21 kwa Singida Fountain Gate FC, Singida FG walikuwa na mwanzo bora sana wa msimu wakiwa na matokeo mazuri na uchezaji unaovutia kwa mtazamaji yoyote yule ila tokea kurejea kwa Ligi baada ya mapumziko mafupi wamekuwa na “Performance” mbaya sana kiwanjani na matokeo pia hayaridhishi, huku kwa upande wa Simba SC wamekuwa na matokeo ambayo hayana muendelezo mzuri wa “Performance” nzuri kiwanjani.
Mpaka sasa timu zote mbili zimekutana Mara tatu kwenye michezo ya Kigi kuu ya NBC tokea Singida FG ipande kwa Mara Ya kwanza 2022/2023, ambapo katika michezo yote mitatu timu zote zilifanikiwa kupata goli bila kujalisha nani aliibuka mshindi mwisho wa mchezo, katika michezo hiyo 3 Simba SC wamefanikiwa kuibuka na ushindi michezo 2 na mmoja ukienda kwa Sare Ya 1-1, huku Simba SC akifunga jumla Ya magoli 6 na kuruhusu 3 dhidi Ya Singida ambapo wachezaji wanaongoza kwa kufunga magoli timu hizi mbili zikikutana ni Saidi Ntibazonkiza wa Simba SC pamoja na Deus Kaseke ambao wote wamefunga magoli mawili kila mmoja.
Takwimu za michezo yao mitano Ya mwisho kwenye Ligi kuu ya NBC ikionyesha Simba SC ikifanikiwa kushinda michezo 3 ikitoa sare moja na kufungwa moja huku wakifunga magoli 6 na wakiruhusu magoli 4, kwa upande wa Singida Fountain Gate FC wao wamefanikiwa kujikusanyia alama moja kwenye michezo mitano Ya mwisho wakifungwa michezo 4 na wakitoa sare mmoja huku wakiruhusu magoli 8 na wakifunga magoli 2 tu.
Simba SC wamekuwa wakitumia wakitumia zaidi mfumo wa 4-2-3-1 wakiwa na viungo wakabaji wawili na wakati mwingine wakiwa na wakabaji watatu, na Mara nyingi wanapoamua kutumia wakabaji wawili huwa wanakuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi tofauti na wakiwa na wakabaji watatu huwa timu inakuwa chini sana na mashambulizi yanakuwa machache, uwepo wa wakabaji wawili Mara nyingi huwa wanampa nafasi kubwa Clatous Chama kuingia ndani na kuipa timu nafasi kubwa ya kutengeneza nafasi za kufunga na wakati mwingine kufunga yeye.
Kwanini uwepo wa Viungo wakabaji watatu hupunguza kasi ya kushambulia?, Mara nyingi huwa anatumika Clatous Chama na Saidi Ntibazonkiza au Kibu Denis kutokea pembeni jambo ambalo linamfanya Sadio Kanoute kuonekana zaidi kwenye 18 ya mpinzani lakini ufanisi wake kwenye kufunga huwa unakuwa Mdogo na hata kutengeneza nafasi huwa haifanyiki ki usahihi na Mara nyingi huwa akitumika Mzamiru Yassin huwa kuna kuwa na kasi ndogo sana Ya kushambulia tofauti na wakimtumia Fabrice Ngoma na Babacar Sarr au Kanoute kama wakabaji basi nafasi nyingi zinatengezwa kwa kuwapa uhuru zaidi Ntibazonkiza, Chama na Kibu kutengeneza nafasi.
Moja Ya udhaifu mkubwa wanaokumbana nao Simba SC ni pale wanapokutana na timu ambayo itaamua kukabia juu kwa kuwapa presha pale wanapomiliki mpira maarufu “Press” huwa wanaacha nafasi kubwa sana na Mara nyingi huwa wakifanyiwa “Caunter attack” inaleta madhara kwenye lango Lao kwanini ?, Mara nyingi wakipanda kushambulia mabeki wao wa pembeni huwa wanaacha “gape” kubwa sana na kuwapa mabeki wa kati kazi kubwa ya kuziziba nafasi zao.
Upande wa Singida FG ndani Ya michezo yao mitano Ya mwisho wamekuwa na “Performance” mbaya sana na hata uchezaji wao hauvutii sana, wamekuwa wakitumia zaidi 4-3-3 wakimtumia Kaseke, Kazadi na Ambundo eneo la juu changamoto kubwa ni pale wakikutana na timu inayoamua kukabia juu wamekuwa wakishindwa kutoka kwenye mtego huo na hiyo imepelekea kuruhusu sana magoli kwenye eneo ilo
Kipi ni kitu bora kwao kuweza kuzuia kufungwa au kuruhusu magoli kwao ?, ni kutumia zaidi kukabia chini“low block” na huwa wakifanya hivyo wanafanikiwa wakiwatumia Andambwile na Kagoma kwenye mfumo wa 4-2-3-1 mbele akibaki Kyombo au Kazadi chini akiwa Deus Kaseke na Gyan ambao wana uwezo wa kusaidia kukaba.
Sasa Nini wafanye ili kuweza kuizuia Simba SC? Jambo kubwa ni kukubali kuwa chini ya Simba nikimaanisha wasitake kufungua mchezo na kupishana na Simba SC itakuwa hatari kwao ukiamua kupishana na Simba ukikosa ufanisi mzuri wa kuzuia basi ni rahisi sana kuruhusu magoli, pili ni kutumia “Caunter attack” na kuwa na usahihi wa kutumia nafasi chache watakazopata ili kufunga magoli na tatu wakimbie zaidi uwanjani kuliko wapinzani wao, matumaini ni kuwa tutashuhudia mchezo mzuri na wenye upinzani kiwanjani.
SOMA ZAIDI: Kwanini Mdhamini Mmoja Timu 6 Ligi Moja?