Wakati macho na masikio ya wengi ni mchezo wa hii leo ambao utaamua hatma ya nani anaungana na Asec Mimosas katika hatua ya robo fainali kumbuka kuwa Simba wanakutana na Jwaneng Galaxy katika uwanja wa Taifa na hapa tumekuandalia orodha ya wachezaji wa kutazamwa kwa jicho la 3 katika mchezo wa hii leo.

1.CLATOUS CHAMA

Mzaliwa wa Ndola, Zambia tokea amekuja nchini na kuhitumikia Simba SC amekuwa muhimili muhimu wa timu hiyo hususa kwenye michezo ya hatua kama hii amekuwa akifanya maamuzi ya mechi kwenye michezo mingi ya CAFCL msimu jana alikuwa na kiwango bora dhidi ya Horoya ya Guinea mechi ambayo iliwapa nafasi ya kufuzu Hatua ya Robo Fainali akifunga magoli na kutengenezea wengine, anapaswa kupewa jicho la Ziada kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Gallaxy.

Pia ikumbukwe ndiyo mchezaji aliyefunga magoli muhimu kuifikisha Simba SC hatua ya makundi msimu huu.

 

2.SAIDI NTIBAZONKIZA

Ni mzaliwa wa Bunjumbura, Burundi akicheza soka la kulipwa Barani Ulaya na kuja nchini ila tokea amejiunga na Simba SC amekuwa mchezaji muhimu kikosini kuanzia kushambulia na hata kuanzisha kukaba kuanzia juu kwa sasa apewi nafasi kubwa ya kufanya maajabu ila uwepo wake uwanjani unaisaidia Simba SC kuanza kukaba kuanzia juu, mpe jicho lako na Jwaneng Gallaxy wanapaswa kumpa umakini mkubwa sana.

 

3.SADIO KANOUTE

Nchini Mali ndiyo ardhi ambayo imempokea kijana huyu ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo, kwa sasa amekuwa mchezaji anayecheza eneo kubwa la uwanja kwenye kikosi cha Simba SC akikaba na kushambulia pia imekuwa ngumu kujua anacheza nafasi gani ikihitajika kukaba basi utamkuta na ikihitajika kusaidia mashambulizi utamkuta. Jwaneng Gallaxy wanapaswa kumchunga sana Sadio Kanoute japo ni ngumu kutokana na namna anavyocheza kwa sasa nampa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huu.

 

4.KIBU DENIS

Hajavuka mipaka ila ni mzaliwa wa Tanzania, amekuwa sehemu ya wachezaji muhimu ndani ya Simba SC nguvu na kasi yake imekuwa kipaumbele kwake kiwanjani hana takwimu bora sana za kufunga na kutengeneza magoli msimu huu ila uwepo wake uwanjani umeisaidia Simba SC, ni moja ya wachezaji wachache kwenye kikosi cha Simba SC ambao wanacheza eneo la ushambuliaji ila utamkuta kwenye eneo la kukaba kusaidia kukaba na eneo la kushambulia pia utamkuta ni ngumu kukabiliana naye na ndiyo maana nampa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

 

5.GOITSEONE PHOKO

Licha ya kuruhusu magoli kwenye michezo yao mitatu ya mwisho ila kipa huyu amekuwa tegemezi na chachu ya Jwaneng Galaxy kumiliki alama nne mpaka sasa kwenye Michuano hii msimu huu, kumbukumbu bora ni mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Simba SC alikuwa kwenye kiwango bora na akiwa sehemu ya kuinyima alama Simba SC kwenye mchezo huo, ni moja ya mchezaji wa kumpa jicho la pili kwenye mtanange huo.

 

6.DANIEL MSENDAMI

Umri wa miaka 23 akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Jwaneng Galaxy ni tegemezi kwenye timu licha ya umri wake mdogo anacheza eneo la ushambuliaji na kwenye mchezo dhidi ya Wydad AC waliyopoteza aliongeza kwa kupiga mashuti 3 yaliyolenga lango peke yake na akiwa na uwezo mzuri wa kupiga pasi huku akiwa na uwezo wa kurudi kusaidia kukaba ni mchezaji wa kuchungwa pia anavaa jezi namba 22.

 

7.NQOBIZITHA MASUKU

Jezi namba 20 mgongoni mwake akiwa na umri wa miaka 30 ni kiungo mkabaji wa Jwaneng Galaxy amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha timu hiyo na ni moja ya wachezaji watatu ambao walikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Wydad AC licha ya kupoteza, ni mzuri kuanzia kupiga pasi fupi na hata pasi ndefu pia amekuwa bora huku akiwa mzuri zaidi kwenye kukaba.

 

8.LESEGO KEREDILWE

Akiwa na umri wa miaka 30 akivaa jezi namba 4 mgongoni anakipiga kwenye eneo la beki tena beki wa kati amekuwa tegemezi kikosini kwani kati ya mabeki wote kikosini yeye amekuwa mzuri kwenye eneo ilo kuanzia kukaba mipira ya chini “tackling” kufanya “recover” amekuwa bora sana zaidi ni kuwa ni mzuri sana kwenye mipira ya juu kuanzia kona pia anauwiano mzuri wa kupiga pasi fupi na ndefu.

SOMA ZAIDI: Niko Sahihi Au Nimemuelewa Vibaya MO DEWJI?

1 Comment

  1. Pingback: Hongereni Wawekezaji Soka Letu Limekua Kwa Kasi - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version