Moja Ya mchezo wenye mvuto ndani yake kwani mchezo huo unakutanisha timu mbili tofauti zenye presha mbili tofauti kwani Simba SC anataka kumaliza nafasi Ya pili akiwa na kiwango kisichoridhisha kwenye michezo 6 mfululizo, huku Mtibwa Sugar akioambana kunasuka mkiani na kucheza hatua Ya mtoano.

Namna timu hizo zinavyocheza zimeonekana zikiwa na matatizo yanayofanana kwani Simba SC wamekuwa na changamoto kubwa kwenye eneo Lao la kuzuia wakiruhusu magoli pamoja na eneo Lao la ushambuliaji kwani wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi za magoli ila wamekuwa wakishindwa kuzitumia, sawa na upande wa Mtibwa Sugar nao wamekuwa wakiruhusu magoli sana hata kama wataibuka na ushindi ila pia wamekuwa wakiruhusu goli sawa na eneo Lao la mwisho wakitengeneza nafasi ila hawazitumii

Takwimu za timu hizo mbili zilipokutana kwenye michezo yao 5 ya mwisho kikosi cha Simba SC kimefanikiwa kushinda michezo 4 na kutoa sare mchezo mmoja huku wakifunga magoli 14 na wakifungwa magoli 2 tu na kikosi cha Mtibwa Sugar. Mchezaji anayeongoza kufunga magoli mengi kwenye michezo hiyo ni Jean Baleke akifunga magoli 4 akifatiwa na Pape Sakho pamoja na Mateo Antony wote wakiwa na magoli 2, hata hivyo wachezaji wote watatu siyo sehemu mchezo huu tena kwani hawapo kwenye timu hizo.

Mchezo huu utakuwa wakivutiwa kiuchezaji kwani timu zote hazitofautiani sana kiuchezaji wamekuwa wakiweka mpira chini na kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma kuelekea eneo Lao la ushambuliaji kwenye lango la mpinzani wake, Mtibwa Sugar wamekuwa wakitumia zaidi mabeki 4 na viungo 4 pia huku wakiwa na washambuliaji wawili ambao ni Seif Karihe pamoja na Charles Ilanfya na wakati mwingi wamekuwa wakibadilika na kutumia mawinga wawili na mshambuliaji mmoja. Huku Simba SC wakiwa wanatumia zaidi mabeki 4 viungo wakabaji wawili na eneo la ushambuliaji wakitumia wachezaji 4, mashambulizi mengi Ya Simba SC yamekuwa yakitengenezwa kupitia eneo Lao la kati “kiungo” kutengeneza nafasi za kufunga magoli.

Mchezo huu eneo ambalo lina hatari zaidi kwa pande zote mbili ni eneo la ushambuliaji hususani kwa Simba SC wamekuwa na wachezaji wazuri kwenye eneo ilo la mwisho la uwanja tofauti na wapinzani wao ambao wamefunga magoli 23 na kuruhusu magoli 39 na kuonyesha kuwa kama Simba SC watakuwa makini ni rahisi kupata goli kwenye mchezo huo.

Eneo lente changamoto kwa timu zote mbili ni eneo la beki kwani timu zote mbili zimekuwa zikiruhusu magoli kirahisi sana mabeki wa timu zote mbili wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao mama ya kuzuia kwa kufanya makosa mengi ambapo wachezaji wa Simba SC kwa kiasi kubwa makosa yao yamekuwa makosa binafsi Ya wachezaji na wakati mwingine kitimu sawa na Mtibwa Sugar.

SOMA ZAIDI: Kinachomponza Mgunda Ni ‘Rangi Yake Na Utanzania Wake’

5 Comments

  1. Officialhd _jr on

    1. Ayoub lakred
    2. Israel mwenda
    3. Mohammed hussein C
    4. Hussein kazi
    5. Chefond malone
    6. Babacar sarr
    7. Edwin balua
    8. Fabrice ngoma
    9. Fred miachael (fred vunja bei)
    10. Ladack chasambi
    11. Luiss miquisson
    Sub
    1. Admin wa kijiweni
    2. Officialhd _jr
    TUNASHINDA NYINGI.

  2. Pingback: Kibu Kuna Muda Ni Lazima Kukubali Kufanya Maamuzi Magumu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version