Klabu ya soka ya wanawake ya Simba ( Simba Queen) imefanikiwa kutwaa Ngao Ya Jamii mwaka 2023 kwa JKT Queens kwa penati 5:4 kufuatia sare ya 1:1 katika uwanja wa Chamazi Complex , Dar Es Salaam.

Katika mchezo huo JKT Queens walitangulia kupata goli dakika ya 15 kupitia kwa Stumai Abdallah kabla ya Simba kusawazisha dakika ya 24 kupitia kwa Danai Bhobho na kuufanya mchezo mpaka kuisha matokeo yakiwa ni bao 1:1.

Kabla ya mchezo huo wa fainali kulikua na mchezo wa kutafuta mshindi wa 3 uliowakutanisha  Yanga Princess dhidi ya Fountain Gate Princess mchezo ambao nao uliamuliwa kwa penati baada ya kuisha kwa bila kufungana na Yanga kuondoka na ushindi wa penati 4:2.

Kukamilika kwa michuano ya Ngao ya Jamii ndio ufunguzi wa ligi kuu ya wanawake ikikaribia kuanza ambapo bingwa mtetezi ni JKT Queens ambaye alichukua msimu uliopita wa 2022/2023.

Kwa taarifa zaidi za michezo na makala mbalimbali unaweza kusoma hapa.

 

Leave A Reply


Exit mobile version