Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya wanawake Tanzania Bara, michuano ya ngao ya jamii ambayo msimu huu imekuja kwa muundo wa vilabu 4 kukutana hatua ya nusu fainali imeendelea katika viwanja vya Chamazi Complex.

Mwaka huu ligi hii fupi ya ligi ya ngao ya jamii imewakutanisha mabingwa watetezi ambao ni JKT QUEENS Pamoja na Simba Queens ambaye alimaliza nafasi ya 2 msimu uliopita wakati Fountain Gate ambao sasa wanaitwa Singida Fountain Gate wakimaliza nafasi ya 3 na Yanga Princess waliomaliza nafasi ya 4.

Katika michezo ya nusu fainali Jkt Queens alikutana na Singida FG na kuwafunga mabao 5 kwa 0 huku Kariakoo Derby kwa upande wa wanawake ikimalizika kwa 0 kwa 0 mchezo ambao ulienda hatua ya penati kwa Simba Queens kuibuka na ushindi wa penati 5 kwa 4 za Yanga Princess.

Kwa matokeo hayo Simba Queens anaenda kukutana na JKT Queens kumtafuta bingwa wa ngao ya jamii huku Yanga Princess wakivaana na Singida FG kumtafuta mshindi wa 3 wa ngao ya Jamii.

Unaifahamu Michezo Hatari Zaidi Duniani? Isome Hapa 

 

Leave A Reply


Exit mobile version