Moja ya makocha ambao watakumbukwa sana ndani ya Simba SC kwa miaka ya karibuni basi ni Patrick Aussems “Uchebe” pamoja na Sven, kumbukumbu bora ua mafanikio ya Simba SC ilitengenezwa na Aussems huku Sven akimalizia msimu bora wa mataji na mpira safi wa kuburudisha.

Aliacha kikosi cha Simba SC kikiwa na furaha ya ushindi wa goli 4-0 dhidi ya FC Platinum na kiwango bora sana kwa kikosi cha timu hiyo ambacho mpaka leo hakijawahi kutokea wala kuonekana tena, namna wachezaji walivyocheza muunganiko bora wa kikosi kuanzia goli, eneo la ulinzi, kiungo mpaka ushambuliaji.

Sven aliitengeneza timu ambayo ilikuwa ikicheza kwa muunganiko na kila mchezaji akifanya majukumu yake kwa usahihi, alitengeneza kikosi ambacho kilikuwa ngumu kuruhusu goli kirahisi na hiyo ilimpa jina kubwa sana nchini.

Licha ya kufanya hayo hakudumu na kikosi cha timu hiyo kwa muda mrefu na hiyo inatupeleka hadi kwenye wasifu wake ambao hautofautiani sana na kocha mpya wa sasa wa Simba SC kwani wakati Sven anaajiriwa Simba SC kama Kocha mkuu alikotoka kote baada ya kuacha kucheza mpira alikuwa Kocha msaidizi ambayo hata Fadlu wa sasa naye ni hivuo hivyo.

Sven alizaliwa Belgium na alikuwa na Leseni ya “Uefa Pro Licence” ambayo ilimuwezesha kufundisha soka eneo lolote duniani,baada ya kutamatisha safari yake ya uchezaji mwaka 2010 aligeukia kwenye ukocha na mwaka 2014 alikuwa msaidizi kwenye kikosi cha Niko Volou hadi 2018 aliendelea kuwa msaidizi kwenye timu kadhaa na alifanikiwa kuchukua ubingwa wa AFCON na kikosi cha Cameroon kabla ya kutangazwa na Simba SC na alikuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1.

Kwa upande wa Fadlu Davids alianza kucheza soka na 2012 aliacha kusakata kabumbu na kuamia kwenye ukocha ambapo mwaka alianza kuwa kocha msaidizi wa Maritzburg akipita vilabu vingine vingi kama msaidizi na mwaka 2023/2024 alikuwa Kocha msaidizi wa kikosi cha Raja Casablanca ambacho walichukua nayo ubingwa wa Ligi kuu Morocco na baada ya hapo alitangazwa kuwa Kocha mkuu wa kikosi cha Dimba SC huku pia nawe akipendelea zaidi mfumo wa 4-2-3-1.

Safari yake na Sven Vandenbroeck haina tofauti kubwa sana na wote wanatangazwa kuwa makocha wa Simba SC huku wakiwa hawana jina kubwa kwenye uoande wa Soka Barani Afrika, kumbukumbu nzuri kwa upande wa Sven ni kuwa baada ya kuachana na timu hiyo alifundisha vilabu kadhaa vikubwa Afrika FAR Rabat, CR Belouzdad, Wydad AC na sasa ni Kocha mkuu wa timu ya Zulte Waregem inayoshiriki Ligi kuu ya Ubelgiji.

Ni wakati sasa kusubiri kuona aliyofanya Sven Vandenbroeck na Simba SC na Fadlu Davids akiyafanya na baada ya hapo kuwa Kocha mkubwa barani Afrika na kupelekea kupata nafasi ya kufundisha vilabu vikubwa, jibu pekee ni swala la muda kusubiri utudhihirishie ilo na kutujibia swali letu Simba SC ni daraja kwa makocha kuoata umaarufu?

SOMA ZAIDI: Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

7 Comments

  1. Nyui wahuni waongo sana mnasema eti mikeka ni ya kweli kumbe hola mnataka kutupiga ela zetu sio poa wazeee afu mnasema kiniwr kina ongea hamna lolote kama mtu binafsi naweza suka mikeka inayo eleweka bora mbaki na mikeka yenu tuu

    • Habari Mwana Kijiweni… Sisi tunaweka mategemeo ya mkeka na wala hatutoi codes bali tunaweka Tips za jinsi unaweza suka mkeka wako na una uhuru wa kubadilisha kwa kile ambacho sisi tunakua tumepost kwenye MKEKA WA LEO endelea kuwa Kijiweni kwani hapa Mtaa Unaongea

Leave A Reply


Exit mobile version