Kesi ya washambuliaji kwa sasa ni jambo gumu linaloisumbua dunia ya mpira, zamani ilikuwa rahisi kuwapata wapachikaji wa mabao lakini siku zinavyozidi kusonga imeongeza ugumu zaidi na hata ukiangalia timu zetu Simba na Yanga.
Chelsea ilikuwa na Didier Drogba, Manchester United na Van magoli huku Liverpool wao walikuwa na Fernando Torres. Hii ilikuwa Dunia ya mpira na tulifurahi sana wakati ule. Nenda Chelsea ya sasa, Manchester United yenyewe Kisha malizia na Liverpool wanavyohangaika kutafuta washambuliaji.
Nikirudi kwenye vilabu vyetu vya Simba na Yanga nao hali ni hiyohiyo kwani ukimtazama huyu Freddy Michael namuona akiwataka mashabiki wake waendelee kumsubiri sana, siyo aina ya wale washambuliaji hatari sana kwenye boksi kwani haogopeshi mabeki wala kuwapa uoga.
Tangu afunge lile goli lake dhidi ya Tabora United, sioni tena ule uwezo wake ni kama ngoma imeanza kuwa ngumu na kutufanya tuendelee kuona washambuliaji ni dunia nyingine kwa sasa, kama utampata inahitajika kumtunza na siyo kumuuza.
Tuko katika kipindi ambacho klabu zetu zinarudi katika michuano ya mabingwa barani Afrika na wakiwa katika hatua mabyo bila shaka kila mmoja anatamani kuingia hatua ya robo fainali kwanza kwa Simba ambao washaingia mara kadhaa pamoja na klabu ya Yanga ambayo wanapambania kuingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika histori ya timu yao.
Wanachokipitia Simba unaweza kusema ndicho ambacho wanapitia Yanga kwani wamekua na changamoto msimu huu ya kupata mshambuliaji hatari wa kufunga magoli kama ambavyo alikua akifanya mshambuliaji wao Mayele, kwa kiasi kikubwa msimu huu magoli mengi ya Yanga yamefungwa na viungo wao hii ni kuonesha kuwa wana wakati mgumu katika upande huu wa ushambuliaji.
Nadhani ni wakati sasa wa klabu za Simba na Yanga kufikiria upya kuhusu bajeti zao haswa katika kutafuta washambuliaji wa timu zao kwani ndio mojawapo ya silaha kubwa kwa ajili ya kufanikiwa katika mechi za kimataifa za ngazi ya klabu.
SOMA ZAIDI: Ratiba Kamili Ya Mwezi Wa Pili Ligi Ya Mabingwa Afrika
1 Comment
Pingback: Hii Ndio Ligi Yetu? Tubadilike Kama Tunataka Mafanikio Kimataifa - Kijiweni