Baada ya dirisha dogo la usajili Tanzania bara kufungwa na timu kadhaa zikiwa zimekwishafanya maboresho kadha wa kadha katika vikosi vyao kumeibuka mada nzito ambayo imekua ikijadiliwa katika vijiwe vya soka kuhusu usajili ambao klabu zetu kubwa za Simba na Yanga umeufanya mpaka sasa.

Ukitazama kuanzia namna ambayo wametumia kufanya skauti na kutazama wachezaji watakaozitumikia timu hizi kumekua na ukakasi mkubwa sana kusema unafanyika usajili wa kimkakati kwani kuna muda mpira wetu siuoni kama kweli utatoka tulipo kwenda sehemu nyingine kutokana na kutawaliwa na ushabiki uliovitawala vilabu hivi vikubwa Afrika Mashariki.

Mfano, ukiutazama usajili unaofanyika ni kama hatujiandai zaidi kwa ajili ya Kwenda kupambana kimataifa zaidi sana kwa ajili ya kusumbuana katika ligi yetu ya ndani. Tazama  timu kama simba inaenda kusajili mchezaji kama Babaccar Sarr kama ulikua hujui huyu ni mchezaji ambae hajacheza miezi mitatu tena unampa miaka miwili kwanini hata usimsajili kwa mkopo kwanza ili ujiridhishe na kiwango chake mfano huyu jamaa mimi sioni akiwazidi chochote aliowakuta katika timu kwenye nafasi hiyo yaani Mzamiru, Ngoma na Kanoute sasa ana faida gani labda?

Kuna tetesi zinataja kuwa Baleke na Phiri wanaondoka unaleta wachezaji wapya kutoka ligi tofauti unajuaje wanakuja kuitika kwenye ligi husika wakati Fredy na Jobe siwezi kuwasema vibaya ila tuna uhakika gani wataendana na ligi yetu sina shaka sana na Fredy kwa maana katoka Zambia mazingira yetu yanafanana sana kuna muda pale simba sioni kama kuna mkakati wa kuboresha timu bali naona wanafanya ili mashabiki waridhike mfano Phiri simba yenyewe ndio imemharibu yule ni mchezaji wa daraja la juu sana kwenye huu ukanda wetu.

Ukiwatazama Watoto wa Jangwani (Yanga) nao ni wale wale unamtoa mtu kama Moloko unamleta Okra ilihali kocha aliepo hana hata mpango wa kutumia mawinga sasa unajiuliza huu ni mpango mkakati wa maendeleo ya timu au ni kwamba wanafanya ili nao waonekane wamesajili binafsi yangu klabu kama Yanga niliona imejikamilisha ingesubiri dirisha kubwa huku hili dogo ingewatazamia zaidi wachezaji wa ndani tu.

Natamani kuona Simba na Yanga zikishindana katika biashara kama ilivyo kwa Real Madrid na Barcelona huko Hispania ila sio kwa hizi tikitaka za bongo hatutotoboa tunataka tukashindane na waarabu basi tusajili kama wao wafanyavyo ila siyo kwa hizi propaganda zinazofayika.

Endelea kusoma zaidi makala mbalimbali tunazoandika hapa kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version