Timu zetu zote (Yanga na Simba) zimetolewa zote kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika (CAF Champion League), klabu ya Yanga imetolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini kwa jumla ya penati 3-2 baada ya matokeo ya jumla kuwa 0-0, huku klabu ya Simba imetolewa na Al Alhy ya Misri kwa jumla ya magoli 3-0.

Sio mbaya hatuna budi ya kuzipongeza sana vilabu vyetu kwa kazi kubwa waliyoifanya mimi  naamini tumekaribia kwenye neema kwa vikosi hivi na mabechi ya ufundi yalivyo nusu fainali au fainali tutaifikia hivi karibuni vilabu vyetu vinatakiwa kusajili wachezaji wa maana tu kwa ajili ya msimu ujao.

Ukiangalia michezo ya jana kidogo tu Yanga ifuzu nusu fainali kama sio yaliyotokea jana walipambana mpaka tone la mwisho pamoja na hayo mpira wetu umekua sana timu kama Mamelodi imefuzu kwa msaada wa VAR tena dhidi ya Yanga ya Tanzania watanzania wote tunatakiwa kujivunia sana kuwa na Yanga.

Simba nao walipambana sana wamefungwa Ila ukiangalia mchezo walicheza vizuri mno kimbinu kilichobaki ni kufunga tu lakini mchezo walitawala sana kwa dakika zote matokeo ya kufungwa 1-0 nyumbani ndio yaliwahukumu Simba kimbinu na kila kitu ndio maana Al Alhy walicheza kufuzu tu mengine hawakutaka.

Kama nchi tumebaki na pointi zetu 71 kwenye Association ranking nafasi ya 6 sio mbaya tupo mahali pazuri, Simba inaendelea kubaki nafasi ya 5 kwenye Club ranking ikiwa na pointi 39 na inaweza kushuka kwa nafasi moja iwapo Petro Luanda ikifuzu nusu fainali, Yanga imebaki nafasi ya 12 kwenye club ranking na pointi 31 inaweza kushuka kwa nafasi moja au mbili iwapo Asec na USM Alger zikifuzu nusu fainali.

SOMA ZAIDI: Simba Ikishindwa Kufuzu Nusu Fainali Uongozi Uwajibike?

3 Comments

  1. Pingback: Al Ahly Na Maajabu Ya Jezi Namba 72 Kabla Ya Mechi

Leave A Reply


Exit mobile version