Kuna wakati maswali mengi yanakuja juu ya hawa wanaofanya usajili kwenye kikosi cha SIMBASC kwani ukweli kwa mtazamo wa nje unaona makosa ya wazi yanafanywa na uongozi wa simba nyakati za kufanya sajili zenye tija kwa klabu na badala yake kuwa na mapambio yasiyo na msingi kwa wachezaji hawa wanaosajiliwa.

Nadhani nitakua sahihi kusema kuwa bado Simba haifanyi usajili wa kuivusha kwenda hatua ya nusu fainali na kwa namna hii itabaki na kuendelea kuwa ndoto ambayo kila mmoja anaiwazia ya kwenda nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Siku zote tuambiane ukweli kuwa siasa na mpira ni vitu viwili tofauti ni matusi makubwa kwa Simba kufeli mtihani mmoja zaidi ya mara Kuzingatia uwajibikaji katika usajili kunaweza kuleta matokeo chanya kwa Simba SC na kwa soka la Tanzania kwa ujumla. Kwanza, itaimarisha imani ya mashabiki na wadau wa soka kwa uongozi wa klabu na kwa ujumla soka la Tanzania. Pili, itasaidia kukuza vipaji vya wachezaji wenye uwezo na kuhakikisha kwamba kikosi cha Simba SC kinakuwa imara na cha ushindani zaidi katika mashindano ya kitaifa na kimataifa. Aidha, uwajibikaji katika usajili unaweza kusaidia kujenga taswira nzuri ya soka la Tanzania kimataifa, hivyo kuwavutia wachezaji na wawekezaji wa kimataifa kushirikiana na klabu zetu.

Sasa kama kweli kunania ya kwenda nusu fainali inatakiwa uongozi wa Simba wabadilike kwenye kufanya usajili na kuamua kuianza na Simba ambayo watu watakua na Imani nayo ambayo itawafanya mashabiki waipende na kuikubali zaidi timu yao.

Mashabiki wanatamani kuona mabadiliko na mafanikio katika michuano ya kimataifa na viongozi wanapaswa kuamini kuwa robo fainali sio kitu cha kujivunia kwani kama timu imekwama hapo muda mrefu sana.

SOMA ZAIDI: Kwanini Yanga vs Mamelodi Na Sio Simba vs Al Ahly?

1 Comment

  1. Pingback: Simba Na Yanga Mmejifunza Nini Ligi Ya Mabingwa? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version