Wakiwa katika uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan klabu ya Sevilla hii leo wana kibarua kigumu cha kukutana na Athletic Bilbao katika mchezo wa ligi kuu ya Hispani almaarufu kama La Liga.

Sevilla wakiwa katika nafasi ya 16 na alama zao 16 katika msimamo wa La Liga wanapitia wakati mgumu zaidi katika ligi hiyo kwani katika mechi zao 5 za mwisho kabla ya kukutana na Bilbao hii leo wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Granada kwa mabao 3:0 na kupoteza michezo 4 dhidi ya Atletico Madrid 1:0, Getafe 3:0, Lens 2:1 na Mallorca bao 1:0.

Bilbao wao wako nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 35 katika mechi 18 walizocheza  na katika mechi zao 5 za mwisho wameshinda mechi 4 dhidi ya Las Palmas 1:0, Atl Madrid 2:0, Cayon 3:0 , Rayo 4:0 na sare ya bao 1:1 dhidi ya Granada.

Toka mwaka 2021 ni mechi ambayo imekua haina idadi kubwa ya magoli wanapokutana vigogo hawa kutoka La Liga licha ya matokeo mabovu waliyonayo Sevilla mpaka sasa katika ligi.

VIDOKEZO VYA UBASHIRI

Muendelezo mzuri wa matokeo kutoka kwa Bilbao ni wazi Sevilla anapoteza mchezo huu ( Atl Bilbao Win)

Mechi haitakua na magoli zaidi ya manne yaani Under 3.5

Kwa wale wanaopenda kubashiri kuhusu card ni kuwa hakutakua na card nyekundu ( Player to be sent off by redcard NO)

Mechi hii Sevilla watashambuliwa sana tutegmee coner zaidi ya 4 kipindi cha kwanza ( First Half Over 3.5 Corners)

Endelea kufuatilia zaidi kuhusu dondoo mbalimbali za mikeka na vidokezo vya ubashiri kwa kugusa hapa.

1 Comment

  1. Pingback: Crystal Palace vs Everton : Ubashiri Na Vidokezo Vya Mkeka - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version