Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samata, ameendelea kuandika historia mpya katika ulimwengu wa soka baada ya klabu yake ya PAOK kutoka ligi kuu ya Ugiriki anayoichezea kwa sasa kutinga Robo fainali katika michuano ya UEFA Conference League wakiwa vinara kutoka kundi G.

PAOK wamekusanya alama 16 na kuwa wababe mbele ya Eintracht Frankfurt wababe wa Bayern baada ya PAOK kuichapa HJK mabao 4-2 na kutinga hatua inayofuata katika michuano hii.

Kufuatia kutinga robo fainali kwa PAOK kumemfanya Mbwana Samatta kuweka rekodi zifuatazo:

1. Samata alikuwa Mtanzania wa kwanza kutinga Robo fainali UEFA Europe League.

2. Samata anakuwa Mtanzania 🇹🇿 wa kwanza kutinga 16 Bora UEFA Conference League

3. Samata alikuwa Mtanzania 🇹🇿 wa kwanza kucheza UEFA Champions League.

4. Samata ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Pendwa Duniani Premier League.

5. Samata alikuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa tuzo kubwa hapa Afrika  inayo simamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Mchezaji bora wa Ligi za Ndani .

Unatamani Samatta aweke rekodi gani kubwa zaidi duniani? Endelea kusoma makala zetu mbalimbali kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version