Sasa baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu Ubelgiji, kocha wa KRC Genk, Wouter Vrancken ameripotiwa kushikilia hatma ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwenye kikosi hicho kufuatia muda wake wa mkopo kumalizika.

Samatta alirejea Genk kwa mikopo wa msimu mzima huku kukiwa na kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja ikiwa watalidhishwa na kiwango chake.

Vrancken ambaye ameiongoza KRC Genk kumaliza msimu ikishika nafasi ya pili ambayo itawafanya msimu ujao kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndiye anayesikiliziwa na mabosi wa timu hiyo.

Kocha huyo, anatarajiwa kuwa na kikao ambacho kitahusisha mwenendo wa klabu ikiwemo  kujadili mipango ya msimu ujao.
Kama wataamua kuachana na mpango wa kumsajili jumla nahodha huyo wa Taifa Stars itambidi arejee Fenerbahce ya Uturuki.

Mkataba wa Samatta na Fenerbahce unatarajiwa kumalizika Jun 30, 2024.

Kwa taarifa za usajili zaidi tufuatilie hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version