Kiungo wa klabu ya Simba, Sadio Kanoute ataukosa mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Athletic Club. Kanoute ataukosa mchezo huo baada ya kupata kadi kwenye mchezo wa jana ambapo inapelekea jumla ya kadi tatu za njano kwenye mechi tatu zilizofuatana, hivyo kikanuni kwenye CAF atakosa mchezo unaofuata.

Sadio alipata kadi katika mchezo wa Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy lakini pia mechi iliyofuata dhidi ya ASEC Mimosa alipata kadi na mchezo dhidi ya Wydad Casablanca inayomfanya kupata kadi 3 mfululizo katika mechi 3 zinazofuatana.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF zinasema Mchezaji atakayepata kadi 3 za njano katika mechi zinazofuatana atakosa mchezo unaofauta.

Kwa taarifa zaidi za michuano ya bara la Afrika unaweza kusoma hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version