Wakazi wa Mkoa wa Iringa na maeneo jirani wamehimizwa kujitokeza kushiriki mbio za RUAHA GREAT MARATHON zitakazofanyika Disemba 16, 2023 kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, (ACP) Allan Bukumbi amesema kuwa Iringa ni shwari na salama hivyo amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo.

Mbio hizo zitaanza mapema kabisa Alfajiri ambazo zitahusisha kukimbia  Kilometa 5 pamoja na Kilometa 10 ambazo lengo kubwa ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya Utalii lakini pia kulinda vyanzo vya maji.

Aidha Kamanda Bukumbi amewaasa wakazi wa Iringa kushiriki kwani ni moja kati ya njia ya kulinda afya zao na kukuza Uchumi wa utalii mkoa wa Iringa.

Mbio hizo ambazo zitaanza na kuhitimishwa katika uwanja wa Samora hazitakua na kiingilio hivyo ni bure kwa wana Iringa Kwenda kushiriki.

Unaweza kuendelea kusoma zaidi habari zetu kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version