MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Garth Crooks, amedai kuwa kumuondoa fowadi Cristiano Ronaldo ndio msingi wa mabadiliko ya klabu hiyo chini ya Erik ten Hag msimu huu.

Manchester United wamepanda hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali la Premier League kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Nottingham Forest Jumapili.

Mabao kutoka kwa Antony na Diogo Dalot yaliwapa vijana wa Ten Hag ushindi kwenye Uwanja wa City Ground.

“Manchester United ilikuwa mojawapo ya timu chache ambazo hazijafungana wikendi hii, lakini kilichokuwa cha pekee ni kwamba United imeharibiwa na majeraha,” Crooks aliandika katika safu yake ya BBC Sport.

“Shukrani zote kwa Erik ten Hag, ambaye hajabadilisha tu timu bali kikosi kizima tangu Cristiano Ronaldo kuondoka.

“Kumuondoa Ronaldo ilikuwa muhimu kwa hilo.”

Ronaldo aliondoka Man United na kujiunga na Al-Nassr kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Man United kuvunjwa kwa makubaliano.

Leave A Reply


Exit mobile version