Kombe la Soka la Afrika (AFL) linajitokeza kwa mara ya kwanza na hatua ya robo fainali imezua michezo mikali kati ya vilabu vikubwa vya bara hili.

Simba SC ya Tanzania itakuwa mwenyeji wa mabingwa wa Misri, Al Ahly, katika mechi ya kwanza ya robo fainali itakayopigwa tarehe 20 Oktoba, kulingana na droo iliyofanywa Jumamosi na Asamoah Gyan, nyota kutoka Ghana, na Maria Borges, mwanamitindo kutoka Angola.

Al Ahly wameshinda taji la TotalEnergies CAF Champions League mara 11, wakati Simba inatafuta kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza katika AFL.

TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waliowahi kushinda taji la Champions League mara tano, watakutana na Esperance ya Tunisia, ambao wamejipatia taji hilo mara nne, katika mechi ya kwanza ya robo fainali tarehe 21 Oktoba.

Klabu ya Nigeria, Enyimba, ambayo ilikuwa klabu ya kwanza ya Nigeria kushinda TotalEnergies CAF Champions League mwaka 2003 na 2004, itakutana na Wydad Casablanca ya Morocco, ambao wameshinda taji hilo mara tatu.

Petro du Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini watakamilisha mechi za robo fainali.

Hata hivyo, ushiriki wa Petro utategemea rufaa waliyoifungua kwa Chama cha Soka cha Angola kuhusu suala la nidhamu.

Mechi za kwanza za robo fainali zitafanyika kuanzia tarehe 20-22 Oktoba, na mechi za marudiano zimepangwa kufanyika kati ya tarehe 24-25 Oktoba ili kutoa washindi wa nusu fainali.

Fainali ya kwanza ya AFL itafanyika mapema Novemba ili kutangaza mabingwa wapya wa Afrika.

Mechi hizi za robo fainali zinakutanisha vilabu vyenye jumla ya mataji 43 ya Champions League, kwenye pambano la mabingwa wa bara hili.

AFL inaahidi kuwa na michezo ya kusisimua kati ya vilabu vya Afrika vyenye sifa kubwa katika soka ya vilabu.

Michezo kamili:

Robo Fainali 1 

Oktoba 20: Simba vs Al-Ahly

Oktoba 24: Al-Ahly vs Simba.

Robo Fainali 2 

Oktoba 21: T.P Mazembe vs Esperance

Oktoba 25: Esperance vs T.P Mazembe.

Robo Fainali 3 

Oktoba 22: Enyimba vs Waydad Casablanca

Oktoba 25: Waydad vs Enyimba.

Robo Fainali 4 

Oktoba 21: Petro Atletico du Luanda vs Mamelodi Sundowns

Oktoba 24: Mamelodi Sundowns vs Petro Atletico du Luanda.

Oktoba 29 na Novemba 1 – Nusu Fainali 1 na Nusu Fainali 2.

Novemba 5 na Novemba 11 – Fainali 1 na Fainali 2.

Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa

Leave A Reply


Exit mobile version