Maswali na shauku kubwa hivi sasa kutoka nyumbani Tanzania ni michezo ya mkondo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya robo fainali ambayo itaamua nani anaenda hatua ya nusu fainali kumbuka kuwa Tanzania inawakilishwa na klabu 2 ambazo ni Simba pamoja na Yanga.
Wakiwa nchini Afrika Kusini, Wananchi yaani klabu ya Yanga wanakutana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa pili baada ya mchezo wa kwanza kuisha kwa suluhu katikauwanja wa Benjamin Mkapa.
Wekundu wa msimbazi wao wako nchini Misri kuvaana na Al Ahly moja kati ya mechi ambayo pia inasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na jinsi ambavyo mchezo unaozikutanisha timu hizi unavyokua na magoli mengi.
Hapa tumekuandalia rekodi zao timu zote wakiwa ugenini na wale ambao wakiwa nyumbani zisome hapa kisha tuachie comments yako hapo chini:
Mamelodi Sundowns wakiwa nyumbani mechi 5 za mwisho CAF
🤝 2-2 Wydad
✅ 2-0 Bumamuru
✅ 3-0 Noudhibou
🤝 0-0 Pyramids
✅ 1-0 Mazembe
YANGA wakiwa Ugenini mechi 3 za mwisho CAF
Belouizdad 3-0 Yanga
Medeama 1-1 Yanga
Al Ahly 1-0 Yanga
AL AHLY wakiwa nyumbani mechi 5 za mwisho CAF
✅ 2-1 Wydad
✅ 4-0 St George
✅ 3-0 Medeama
🤝 0-0 Belouizdad
✅ 1-0 Yanga
SIMBA SC wakiwa Ugenini mechi 3 za mwisho CAF
🤝 Jwaneng 0-0 Simba
❌ Wydad 1-0 Simba
🤝 Asec 0-0 Simba
SOMA ZAIDI: Barua Hii Iwafikie Wachezaji Wa Simba Huko Misri
1 Comment
Sawia