HATIMAYE Bodi ya Ligi wametangaza Ratiba ya Msimu wa Ligi Kuu 2024/25 ambayo itaanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 16 kwa mchezo mmoja pekee, huku Simba wakifungua Ligi tarehe 18 dhidi ya Tabaora Utd.

Simba SC watafungua msimu wao pale KMC Complex, ambapo inaelezwa kuwa wamechagua kutumia uwanja wa KMC Complex pale Mwenge kwa michezo yake ya nyumbani , lakini mechi kubwa zote zitapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bingwa Mtetezi wa Ligi kuu ya NBC Yanga SC, wataanza kuusaka Ubingwa wa 4 mfululizo kule mkoani Kagera katika Dimba la Kaitaba, kisha watarejea Azam Complex ambapo watapatumia kama Uwanja wa nyumbani pia kwa msimu huu kwa sehemu kubwa ya mechi zao.

Azam FC wao wataanzia kwa Mej.Jen. Isamhuyo vs JKT Tanzania.

MECHI 10 ZA AWALI ZA SIMBA SC 2024/25

Simba vs Tabora Utd

Simba vs Fountain Gate

Tz Prisons vs Simba

Azam FC vs Simba

Simba vs Namungo

Dodoma Jiji vs Simba

Simba vs Coastal Union

Simba vs Yanga Okt 19

Mashujaa FC vs Simba

Simba vs JKT Tanzania.

MECHI 10 ZA AWALI ZA YANGA SC 2024/25

Kagera Sugar vs Yanga

KenGold FC vs Yanga

Yanga vs JKT Tanzania

Yanga vs Mashujaa FC

Singida BS vs Yanga

Yanga vs KMC FC.

Yanga vs Pamba Jiji

Simba vs Yanga

Yanga vs Tabora Utd

Coastal Union vs Yanga

Mechi kubwa inayotazamwa na wengi ni ya Simba na Yanga ambayo itapigwa Oktoba 19, ikiwa ni mechi ya 8 tangu kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.


SOMA ZAIDI: Huu Ni Mtazamo Wangu Kuhusu Soka Letu

11 Comments

  1. Kama itaonekana basi simba inafungwa Tena kwa kikosi Cha simba basi mm na mpira ndio basiii siwezi kwenda yanga ila Bora niache kushabikia tu💯

  2. Shephani ashel on

    Mshabiki yeyote ambaye hana maslahi natimu, haichangii timu walk hajulikani kwa kiongoz yeyote wa timu kuanzia ngazi ya juu mpaka matawi. Ukihama nisawa na mzazi aliemzaa mtoto kisha mtoto huyo akawa kichaa na akasema huyu sio mwanangu kwasababu ni kichaa.

  3. Marco sabatho on

    Wana Simba SC waendelee kupiga mazoezi ya kutafta muunganiko wa timu maana hata uwanja wa nyumbani tulochagua unaonekana wa ugenini ni bora azam complex stadium..so wachezaji wajitume maradufu ubingwa ni wetu mwaka huu ni wa kufoc.

Leave A Reply


Exit mobile version