Baada ya kusimama kwa takribani siku 40 kupisha mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea nchini Ivory Coast Ligi Kuu ya NBC inarejea tena Februari 2 kwa ratiba ya mchezo mmoja utakaopigwa saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga.

Tuitazame hapa ratiba ngumu ya klabu ya Yanga katika Ligi kuu wakianza kesho dhidi ya Kagera Sugar.

02/02/2024 = Kagera Sugar vs Yanga Sc  

05/02/2024= Yanga Sc vs Dodoma Jiji

08/02/2024 = Yanga Sc vs Mashujaa Fc

11/02/2024= Tanzania Prisons vs Yanga 

17/02/2024= KMV vs Yanga Sc

23-25 /02/2024 = Yanga Sc vs CR Belouizdad 

Katika michuano ya mataifa barani Afrika wachezaji wanaotoka ligi kuu waliobakia kwenye mashindano hayo hadi sasa ni Henock Inonga wa timu ya Simba Pamoja na Djigui Diarra wa Yanga hivyo kuruhusu ligi hiyo kuendelea kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu anayeoongoza ni Azam Fc akiwa na alama 31 katika mechi 13 alizocheza akifuatiwa na Yanga mwenye alama 30 katika mechi 11 alizocheza huku Simba akiwa na michezo 10 na alama 23 pekee. Chini ya msimamo yupo Mtibwa mwenye alama 8 juu yake akiwa Mashujaa mwenye alama 9.

SOMA ZAIDI: Ule muda wa kufanya maajabu Ligi Kuu umerejea.

Leave A Reply


Exit mobile version