Baada ya hatua ya 16 bora michuano ya kombe la mataifa barani Afrika kukamilika ni rasmi sasa presha na joto linazidi kupanda zaidi la michuano hii mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa ambapo tunaangalia ratiba ya robo fainali ya michuano hii. Ukiachilia mbali matokeo ya kushangaza lakini pia kuenguliwa katika michuano hii kwa mataifa bora barani Afrika kisoka na timu za taifa ambazo hazikutarajiwa pia ni moja ya ishara ya kukua kwa soka Afrika.

Ratiba kamili ya michuano hii ya AFCON katika hatua ya robo fainali iko hivi:

02/02/2024

  • Nigeria vs Angola
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) vs Guinea

03/02/2024

  • Mali vs Ivory Coast
  • Cape Verde vs Afrika Kusini

DONDOO:

Kutolewa kwa Morocco na timu ya taifa ya Afrika Kusini maana ake ni kwamba wanajiunga na mabingwa watetezi Senegal, Tunisia, Algeria, Cameroon na Burkina Faso kama timu  zinazoorodheshwa katika nafasi 10 za juu barani Afrika kwa viwango vya FIFA ambazo zimefungasha virago mapema katika michuano ya msimu huu nchini Ivory Coast.

Kumbuka kuwa AFCON ya mwaka huu ni moja ya michuano ambayo imeingia katika historia kubwa zaidi katika historia ya mashindano hayo kutokana na zawadi ambazo zimeandaliwa kwani mabingwa watapokea kitita cha dola milioni 7 ambalo ni ongezeko la asilimia 40 kutoka kwa toleo la awali jambo ambalo mpaka sasa limetufanya tuone michuano ya kuvutia na yenye ushindani mkubwa zaidi kutoka kwa mataifa ambayo hayakutarajiwa kufanya vyema.

SOMA ZAIDI: Waliotegemewa wameduwazwa na wasiotegemewa AFCON 2023

 

 

 

1 Comment

  1. Pingback: Walioleta VAR AFCON Wana Nafasi Yao Moyoni Mwangu - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version