Utakua umeshaimisi tayari na sisi tumekuandalia hapa ratiba kamili ya hatua ya nusu fainali michuano ya kombe la mataifa barani Afrika, nani kutinga hatua ya fainali na kubeba ubingwa wa AFCON kwa mwaka huu ambao timu zilizoingia hatua hii ni wenyeji Ivory Coast, Afrika Kusini, Nigeria na DR Congo. Hii ndio ratiba kamili:
Nigeria vs South Africa
Nusu fainali ya kwanza ni mchezo kati ya Nigeria dhidi ya South Afrika utakaopigwa katika uwanja wa Bouaké. Nigeria ametinga hatua hii baada ya kumtoa Angola kwa kumfunga bao 1:0 lililofungwa na Lookman.
South Africa wameingia hatua hii baada ya kumtoa Cape Verde kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kuisha sare ya bila kufungana dk 120 za mchezo pongezi kubwa zikiwa kwa Mlinda lango wa South Africa alieokoa penati 4.
Mshindi wa mchezo huu anakutana na bingwa wa wa mchezo kati ya Ivory Coast dhidi ya DR Congo.
Ivory Coast vs DR Congo
Wenyeji wa michuano hii walipambana sana katika mchezo huu licha ya kuwa pungufu katika kikosi chao lakini waliweza kulazimisha kwenda dakika 120 na kufunga bao liliowapeleka hatua ya nusu fainali na ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya Mali. Mabao yakifungwa na Simon Adingra na Oumar Diakité. DR Congo wametinga hatua hii kwa kuwafunga Guinea mabao 3:1 mabao ya Chancel Mbemba,Yoane Wissa na Arthur Masuaku huku bao la Guinea likifungwa na Mohammed Bayo.
Mshindi wa mchezo huu atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Nigeria dhidi ya Afrika Kusini.
Watakaofungwa katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza na mchezo wa nusu fainali ya pili watakutana katika mchezo wa kutafuta mshindi wa 3.
SOMA ZAIDI: Safari Ya Afcon Na Heshima Kubwa Kwa Ligi Za Afrika