Rais Samia Suluhu Hassan ameilipia klabu ya Yanga ndege maalumu ya kuwapeleka mkoani Mbeya kucheza michezo yao miwili ya Ligi Kuu Bara kutokana na mwingiliano wa ratiba.

Jana Juni 4, 2023 Mhe. Rais aliwaalika Yanga chakula cha jioni Ikulu leo Jumatatu ambapo ratiba hiyo iliingiliana na safari ya klabu hiyo kuelekea mkoani Mbeya.

Akizungumza katika radio ya Wasafi jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Juni 5, 2023 Rais wa klabu hiyo, Hersi Said amesema kutokana na mwingiliano huo wa ratiba uliotokea Rais Samia ameilipia Yanga ndege maalumu kuwapeleka Mbeya baada ya chakula cha jioni.

“Ndege yetu ambayo tulitakiwa kuondoka nayo kwenda Mbeya ilikuwa ni saa 1 usiku lakini kwasababu ya mwaliko wa Rais Ikulu leo jioni tulimpa taarifa kuhusu safari yetu na sasa amelipia ndege maalumu kutupeleka Mbeya,”amesema Hersi.

Hersi amesema ndege hiyo iliyolipiwa na Rais Samia itaondoka saa 5 usiku baada ya kumaliza mazungumzo na chakula cha jioni.

Yanga atakuwa mkoani Mbeya katika mechi dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kesho Juni 6, na kumalizia na Tanzania Prisons Juni 9, 2023.

Yanga imepata mwaliko huo na Rais Samia baada ya kumaliza mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) mwaka 2022/2023.

Kwa taarifa zaidi tufatilie hapa.

4 Comments

  1. Pingback: CHANETA Imetufikirisha Kuhusu ‘Goli la Mama’ - The Chanzo

  2. Pingback: tadalafil online

  3. Pingback: who can write my essay

  4. Pingback: essay about service

Leave A Reply


Exit mobile version