Ilipoishia “Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone na afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauli yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, maneno aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yangu kwake
“Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile, wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu, Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia, chozi lilikuwa likinivuja. Endelea
SEHEMU YA TISA
Aliingia Bilionea Dhabi, alitukuta tukiwa katikati ya maongezi yetu. Mzee Dhabi aliponiona alitabasamu tuu, alikuwa ameongozana na Mke wake ambaye ni Mama Mzazi wa Osman, Alinisogelea kisha aliniambia
“Jacklin! Hujakosea, upo sahihi, ni ngumu sana kuolewa na Mwanaume ambaye hayupo ndani ya moyo wako, upo sahihi sababu huwezi ndiyo maana uliondoka jana Usiku. Lakini Jacklin, hebu tazama macho ya Mama yake Osman, ona lile chozi kwanza” Niligeuza macho yangu kumtazama Mama yake Osman, Ni kweli alikuwa akivuja mchozi
“Analia kwasababu Osman ni Mtoto wake wa kipekee, hana Mtoto mwingine kama ulivyo wewe kwa Mama yako, lile chozi ndilo ambalo Mama yako alikuwa akilia wakati alipopoteza tumaini la wewe kuishi. Unakumbuka kilichotokea, Mungu alimleta Osman katika Maisha yako, alipambana hata kutoa figo lake ili upone, hakufanya kwa ajili ya mapenzi bali kwa huruma yake kwa Mama yako, ulilala Jacklin hukumuona Mama yako alivyokuwa anahangaika hata kutaka kutoa figo lake akuwekee wewe” Bilionea Dhabi alizungumza maneno mazito sana ambayo yalimfanya Mama ajiinamie akiwa analia
“Nakuomba sana Jacklin, okoa Maisha ya Mwanangu, hatuna Mtoto mwingine zaidi yake, Osman ndiye Maisha yetu, kufa au kupona kwa Osman kunakutegemea wewe Jacklin” Alisema Mzee Dhabi kisha alienda kuketi kando ya Mke wake, maneno yake yalinifanya nishindwe kuendelea kuketi pale sebleni nilikimbilia chumbani kwangu. Ni kweli Osman alijitoa na kuhakikisha Maisha yangu yanarudi, tumaini la Mama yangu linarudi, leo yupo Kitndani na Mimi ndiye ninayepaswa kumuamsha, Daaah roho iliniuma sana.
“Usilie Mama Jacklin, Binti yako ni Mtu mzima anajuwa anachokifanya. Kama amekataa kumsaidia Osman hakuna njia nyingine tutaondoka naye kuelekea Dubai tukajaribu huko, ikishindikana basi haikuwa ridhki yetu kuwa na Osman” Alisema Baba yake Osman, Mama yake Osman alikuwa akilia huku akiwa amejifunika na kitambaa alishindwa hata kusema chochote, Mama yangu alinyanyuka na kunifuata chumbani, alinikuta nikiwa nimeshikilia simu yangu, alisogea kisha aliketi kando yangu kwa upole sana alisema
“Jacklin Mwanangu! Nilikuzaa na kukulea katika Mazingira ya kujuwa nini Maana ya utu na shida, pengine ndiyo nguvu iliyomvuta Osman kuja kwenye Maisha yako, alikuja kama Masia akaokoa Maisha yako, leo amegeuka kikwazo cha furaha yako. Nikiwa kama Mama yako nakueleza jinsi ninavyojisikia Jacklin” Alisema Mama kisha alifikicha jicho lake moja ambalo lilikuwa likimwaga chozi
“Moyo wangu umevunjika Jacklin, furaha imenitoweka kama Kizimikavyo kibatari wakati wa upepo Mkali, Jacklin Mama yako nimeumia sana. Siku Osman akiondoka hapa Duniani ndiyo itakuwa mwisho wako kusikia sauti yangu, yule Kijana alirudisha tumaini kwenye moyo wangu, alinifanya nijisikie amani sana lakini leo umeiondoa yote” Mama alisema, nilitamani kumjibu na Kumwambia kuwa kama nitaolewa na Osman basi Mosses atasambaza video zangu za faragha, hadi Mama anaondoka chumbani kwangu mdomo wangu ulikuwa mzito sana kama samaki aliyejaza maji mengi
Niliangalia ujumbe ambao Mosses aliutuma, alikuwa akinikumbusha kuwa endapo nitamuacha atasambaza hizo video, nilivujisha chozi machoni mwangu. Yalikuwa ni maumivu makali sana ambayo hata sikuwahi kuyahisi katika Maisha yangu. Nilipaswa kuokoa Maisha ya Osman kama ambavyo aliokoa yangu ila ningefanya kitu gani? Kama video zitasambaa naweza hata kujitoa uhai kukwepa aibu nzito lakini je Mama yangu Mzazi akiziona video hizo naye atakuwa katika hali gani? Vipi Familia ya Osman itajisikia vipi, ndio maana nasema kilikuwa ni kipindi kizito na kigumu kwangu.
Mama aliporudi Sebleni hakuwakuta Baba na Mama yake Osman, aliangusha kilio kama kuna Mtu amefariki, nilishtuka na niliumia sana. Nyumba ilikosa ile amani iliyokuwepo Mwanzo, ukimya ulitawala hakuna aliyetoa neno lolote zaidi ya sauti za kufungwa na kufunguliwa kwa milango. Nilijitupa kitandani nikawaza sana nifanye jambo gani ili kumsaida Osman bila kuchukua uamuzi ambao ungesababisha kusambaa kwa video hizo za faragha. Kadili nilivyokuwa natulia kitandani ndivyo picha ya tukio la kukataa kuvishwa pete na Osman lilivyokuwa linajirudia katika akili yangu, nilikosa utulivu kama Mtu anayesumbuliwa na mizimu, niliamka bado Mama alikuwa akiendelea kulia, nikiwa kama Mtoto nilijivuta kwenda kumbembeleza.
Nilimkuta akiwa amekaa chini ameegemea sofa, niliketi kwa adabu na utulivu mkubwa sana, Mama alihisi ujio wangu alitulia kimya huku akihema sana. Nilishusha pumzi zangu kisha nilisema
“Samahani Mama najuwa nimekuvunja moyo ila..” Kabla hata sijamaliza nilichokitaka kukisema Mama alinikatisha
“Ishia hapo hapo Jacklin, Wazazi ambao Mtoto wao aliokoa uhai wako wameondoka kwasababu umekataa kuokoa uhai wa Mtoto wao, nimeonekana Mama mbaya sana, Mama mbinafsi ambaye hajali kuhusu Mtoto wa mwingine” Alisema Mama kisha aliendelea
“Kama Osman atakufa basi juwa ni kwasababu yako, hupaswi kusameheka katika hilo Jacklin” Alimaliza kusema kisha alinyanyuka na kwenda zake chumbani kwake, chozi lilinimwagika Mimi Jacklin niliona kila Kiti kipo dhidi yangu, sikuwa na Mtu wa kunisemea kabisa.
Usiku ulipofika niliondoka nyumbani nilienda kulala Hotelini, nilihitaji muda wa kuwa peke yangu ili niweze kutafakari mambo kwa umakini zaidi. Nilizima simu zangu ili nisipate usumbufu wowote ule, hakuna aliyejuwa niko wapi, Si Mosses wala Mama yangu niliyemwambia, nilitaka kutafakari ili nijuwe nafanya nini katika kipindi kigumu kama hiki.
Hali ya Osman haikuwa nzuri kabisa kule Hospitalini, alikuwa kila azindukapo anataja jina langu tu, alikuwa anachomwa sindano za usingizi ili kumtuliza. Familia ya Bilionea Dhabi iliingia gizani, tumaini lao juu yangu liliondoka kabisa, wakiwa nyumbani kwao Mke wa Bilionea Dhabi alimwambia Mume wake
“Twende kwa mara ya mwisho kuzungumza na Jacklin kama atakataa kwa kinywa chake basi hatutokuwa na namna nyingine bali kuondoka na Osman” Alisema kwa sauti ya Kimama iliyojaa maumivu ya kumuona Mtoto wake akiwa kitandani na hana tumaini lolote lile
“Sasa hata kama tutafanya hivyo Mama Osman, Binti hawezi badili msimamo wake, hampendi Osman na hilo lipo wazi sana” Alijibu Baba yake Osman, Mara mlango uligongwa
“Ingia” Alisema Bilionea Dhabi baada ya kumtambua aliyekuwa akigonga, alikuwa ni Mlinzi
“Samahani Baba na Mama, kuna mgeni hapo nje anasema anahitaji kuonana na Osman” Alisema Mlinzi huyo baada ya kuwa tayari ameingia ndani, Mzee Dhabi aliangalia saa yake aliona ni mishale ya saa 4 za Usiku alimuuliza Mlinzi
“Huyo Mtu yupoje?”
“Mwanamke, mweupe” Alisema Mlinzi kisha alitabasamu tu baada ya alichotaka kukisema kuhisi hakina maana hapo mbele ya Mzee Dhabi na Mke wake lakini Mzee Dhabi alimuelewa Mlinzi akamrahisishia
“Mzuri Eeh” Basi mlinzi alitoa tabasamu zito
“Mh! Atakuwa Nani huyo!” Alisema Bilionea Dhabi kisha alitafakari
“Utamjuwa vipi bila kumuona, Mlete” Alidakia Mke wa Mzee Dhabi. Mara moja Mlinzi aliondoka, dakika moja baadaye alirudi akiwa ameambatana na Mgeni huyo
Mzee Dhabi na Mke wake walisimama kwa Mshangao Mkubwa sana baada ya kumuona Mgeni huyo kisha Mzee Dhabi alisema
“Mlinzi nenda” Mlinzi aliondoka zake
- •••••••••••••••••••••••••••
“Zahra?”
“Zahra?” Mzee Dhabi na Mke wake alisema kwa pamoja baada ya kumuona Zahra mbele yao, Si unamkumbuka Zahra? Ni yule Mwanamke aliyechota kiasi kikubwa cha pesa na kutimkia zake Ughaibuni, alikuwa ni mpenzi wa Osman ambaye aliuteka moyo wa Osman miezi kadhaa iliyopita aliondoka na kusema kuwa ana Mwanaume mwingine hivyo Osman asihangaike kumtafuta, tukio hilo lilisababisha Osman kupata Mshituko na kukimbizwa Hospitalini.
Zahra alishtuka kuwaona Wazazi wa Osman, alitetemeka kwa Hofu
“Hebu keti” Alisema Mzee Dhabi, wote waliketi kisha Mzee Dhabi na Mke wake walitazamana
“Ni wewe Zahra au tunaota ndoto ya Mchana?” Aliuliza Mama yake Osman
“Ni Mimi Mama naomba msamaha wenu kwa kila kilichotokea, natamani kumuomba msamaha Osman na ndiyo sababu ya kuja hapa” Alisema Zahra
“Unataka kumuomba Msamaha Osman?”
“Ndiyo Baba! Najuta kwa kila nilichomfanyia.
“Nifuate” Alisema Mzee Dhabi, walitoka ndani Bilionea Dhabi na Zahra, waliingia kwenye gari ya kifahari ya Mzee huyo kisha safari ilianza, Zahra hakujuwa alikuwa akipelekwa wapi
“Baba tunaenda wapi?” Alihoji Zahra
“Si umesema unataka kumuomba msamaha Osman? ”
“Ndiyo Baba”
“Tunaenda alipo Osman”
Usiku huo nilikuwa nimeamua jambo moja, kumsaidia Osman kwasababu alisaidia Maisha yangu, akili yangu iliniambia kuwa Osman alikuwa mwenye huruma na mapenzi ya kweli kuliko Mosses ambaye alianza kutishia kusambaza video zangu za Faragha. Niliondoka Hotelini nikaelekea nyumbani, Nilipochungulia ndani nilimuona Mama akiwa amekaa kando ya Mlango wa kuingilia ndani nilijuwa tu alikuwa akinitafuta japo alinichunia, nilitabasamu sababu Mama yangu alikuwa ni Mama mwenye upendo wa Hali ya juu sana kwangu, nilifuangua geti, nilitupa macho upande wa kushoto nililiona lile gari aliloninunulia Osman kwenye siku yangu ya Kuzaliwa, moyo uliniuma sana.
Nilisogea alipo Mama kisha nilimwambia
“Mama nipeleke Hospitalini alipo Osman” Kauli yangu ilimfanya Mama anitazame mara mbili mbili
“Mama moyo wangu unaniambia tufanye haraka sana” Nilisema nikiwa kwenye hali ya Haraka, lilikuwa ni jambo ambalo Mama alikuwa akilisubiria. Haraka alikimbilia ndani akatoka na mtandio, tulitoka tukachukua Tax kisha safari ya kuelekea Hospitali ilianza.
Upande wa pili, Baba Osman na Zahra walikuwa wanaingia Hospitalini, walisogeza gari kwenye maegesho kisha walielekea Wodini ambako Osman alikuwepo
“Baba Osman anaumwa? Mbona umenileta Hospitalini?” Aliuliza Zahra
“Ndiyo Osman ni Mgonjwa sana ndiyo maana nimekuleta hapa Zahra” Alijibu Baba Osman, walishuka kisha walielekea ilipo wodi hiyo. Bahati nzuri walikutana na Dokta Simon ambaye alikuwa akitoka wodini humo, alipomuona Zahra alishangaa sana
“Najuwa una maswali mengi Simon lakini hiyo ndiyo hali halisi” alielezea Mzee Dhabi baada ya kuisoma sura ya Dokta Simon ilivyokuwa
“Lakini Mzee, Osman hapaswi kushtushwa na jambo lingine mnaweza kumpoteza kabisa, kwanini aje leo?”
“Maswali yako Simon hayawezi kujibiwa kwasasa, nina imani na hiki atakachokiona Osman” Aliesema Mzee Dhabi
“Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Macho angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisema Dokta Simon
“Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twende Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra, waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simon
Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman, aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa. Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuona Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmke ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
9 Comments
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Dah toa nyingine ata usiku wa leo😭😭
Nimepumua baada ya kumaliza kusoma
Dah naona kesho mbal tuendeleee hadith imejoga sasa apo kwa akili ya haraka haraka julieth akimuona zarha atagoma ten kumhudumia osman 🤞🤞🤞uwiiiiiiiiiiii hadith tam nyie 💔💔💔💔💔💔🤕🤕🤕🤕🤕NATAFTA MPENZ KAMA OSMAN🤕
Lete mbili juzi uliruka
Mshtuko umuue osman wazazi wa osman wamfukuze jack moses amuache jack mama yake ammchukie hyo pumzi itakuwa ya mwsho
Mtunzi apewe maua yake 💐 🌹
Jmn wanawake!!! 🤔🤔 khaa
Sehemu ya nane IPO wapi